UKIUJUA UKWELI UTALIA SANA UONGO UMEFANYWA UKWELI

Hakika ukiujua ukweli lazima utalia.
#Ndugu zangu tumrudie Mwenyezi Mungu  na tumuombe Mwenyezi Mungu atusamahe dhambi zetu na atupe rehema zake maana yeye ni Mwingi wa kurehemu. Huwezi amini kwa jinsi Ibilisi anavyo jigamba kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwapoteza waanadamu. Leo hii kuna wanadamu wamegeuzwa na Ibilisi wakaamusi Mola wao mlezi na kuanza kumtaka msaada asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Hii imetokea ili yatimie maandiko maana imeaandikwa LUKA 21:23 "Ole wao
wenye mimba na watakaoukuwa
wananyonyesha katika siku hizo! Kutakuwa na
dhiki kuu katika nchi na ghadhabu juu ya hawa
watu.
#Hakika Ibilisi amewapovusha wanadamu tazama walivyo potoshwa mpaka wakamuasi ALLAH na wakati kwake sisi sote tutarejea na hukumu itasimama tayari kila mmoja analipwa alichokichuma  duniani. Ole wao siku hiyo walio mshirikisha ALLAH huku wakisema amegawanyika katika utatu! Ole wao wale waliosema huyu ni mwana wa ALLAH wakati yeye hakuzaa wala hafanani na chochote! Ole wao waliomuabudu mtu huku wakisema hakika huyu ndiye nabii na Mungu wetu! Ole wao walio mkataa mtume wa Mwenyezi Mungu Mohammad S.a.w huku wakigeuza ukweli kuwa uongo na wakawa wanaitilifiana wao kwa wao! Ole wao walio ificha Torati na kuwafundisha watu hekima itokayo kwao (Kumbukumbu la Torati) huku wakiwambia watu hizi ndizo sheria za Allah.
#Kama ilivyo andikwa akika Walio mwamini ALLAH na Mtume wake watapigwa na kufukuzwa kwenye masinagogi (misiki) na hakika hakuna Nabii aliyefundisha katika kanisa isipokuwa Manabii wote na Mitume walikuwa wanafundisha Maneno ya ALLAH ndani ya Masinagogi (misikiti) YOHANA 6:59 "Yesu alisema maneno haya alipokuwa
akifundisha katika sinagogi huko Kapernaumu.  Lakini oneni Ibilisi alivyo wapambia wanadamu na kuwatoa ndani ya Masinagogi leo hii wanacheza na kushangilia ndani ya Makanisa na wanashindwa kutambua kuwa hakuna Nabii wala Mtume aliyeingia Kanisani na kitu kanisa wao hawakijui isipokuwa Wanazijua misikiti tu yaani Masinagogi.
#Hakika hakuna Nabii wala Mtume wa ALLAH awezaye kupata laana wala hawezi kupata laana kamwe na ALLAH ni mjuzi wa yote. Lakini Ibilisi amewapotosha wale wote wasemao Nabii kalaniwa na wakawa wanauamini msaraba kuwa ndio ukombozi wao" Lakini wanasahau kuwa Tafsiri ya msalaba ni laana. (Yaani ukiumini msaraba ujue umeamini laana)
#Imeandikwa amelaniwa atundikwaye msalabani wa wauaminio msaraba hakika hii ni laana WAGALATIA3:13 Kristo alitukomboa kutoka katika
laana ya sheria kwa kufanyika laana kwa ajili
yetu, kwa maana imeandikwa, “Amelaaniwa
yeye aangikwaye juu ya mti.
#Je yaweza kuwa kweli Nabii wa ALLAH awe mwenye kulaaniwa??? hakika haiwi ila Ibilisi aliwaongoza wale walio ivunja TORATI na kuiandika KUMBUKUMBU LA TORATI ili mpate kupotea na muingizwe katika ziwa la moto. Kama ilivyo andikwa" wataingizwa katika ziwa la moto wale wote waliomwabudu mtu (mnyama) na alama yake (msaraba) UFUNUO 19:20"Lakini yule mnyama
akakamatwa pamoja na huyo nabii wa uongo
ambaye alikuwa amefanya ishara kwa niaba ya
huyo mnyama, ambaye kwa ishara hizi
aliwadanganya wale waliopokea chapa ya huyo
mnyama na kuiabudu sanamu yake. Hawa
wawili wakatupwa wakiwa hai ndani ya ziwa la
moto liwakalo kwa kiberiti..............................................................................................

#FUMBUA MACHO SASA BALAGUMU LITAPULIZWA MDA WOWOTE.
Daima Angaza inakutakia usomaji mwema na Mwenyezi Mungu akufungua macho ili upate kuona haki na uikimbie batili.
Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment