ADHKARI ZENYE MALIPO MAKUBWA KWA ALLAH PAMOJA NA MATUMIZI (In Shaa Allah ) DANI YA DUA



Adhkaar Zenye Thawabu Maradufu


Zifutazo ni Adhkaar ambazo Muislamu anapozisoma, atajichumia milioni za thawabu  kwa muda usiozidi dakika moja kila moja!  Zote zimetokana na mafunzo Sahihi katika Sunnah.

سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ عَدَدَ خَلْـقِه ، وَرِضـا نَفْسِـه ، وَزِنََـةَ عَـرْشِـه ، وَمِـدادَ كَلِمـاتِـه


SubhaanaLLahi wa Bihamdihi ‘adada Khalqihi wa Ridhwaa Nafsihi wa Ziynata ‘Arshihi wa Midaada Kalimaatihi  (mara 3)



الْحَمْدُ لِلَّهِ عَدَدَ مَا خَلَقَ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ مِلْءَ مَا خَلَقَ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ عَدَدَ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ عَدَدَ مَا أَحْصَى كِتَابُهُ،  وَالْحَمْدُ لِلَّهِ مِلْءَ مَا أَحْصَى كِتَابُهُ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ عَدَدَ كُلِّ شَيْءٍ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ مِلْءَ كُلِّ شَيْءٍ، 

AlhamduliLLaahi ‘adada maa Khalaq, wal-HamduliLLaahi  mil-a maa Khalaq, wal-HamduliLLaahi ‘adada maa fis-samaawati wa maa fil-ardhi, wal-HamduliLLaahi ‘adada maa ahswaa Kitaabuhu, wal-HamduliLLaahi mil-a maa ahswaa Kitaabuhu, wal-HamduliLLaahi ‘adada kulli shay-in, wal-HamduliLlaahi mil-a kulli shay-in. (mara 3)


سُبْحانَ اللهِ عَدَدَ مَا خَلَقَ فِي السَّماءِ , وَ سُبْحانَ اللهِ عَدَدَ مَا خَلَقَ فِي الأَرْضِ,  وَ سُبْحانَ اللهِ عَدَدَ مَا  بَيْنَ ذَلِكَ,   وَ سُبْحانَ اللهِ عَدَدَ مَا هُوَ خَالِقُ , وَ اللهُ أَكْبَرْ مِثْلُ ذَلِكَ, وَالْحَمْدُ لِلَّهِ مِثْلُ ذَلِكَ, وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهَ مِثْلُ ذَلِكَ,  وَ لاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللهِ مِثْلُ ذَلِكَ

Subhaana-Allaah ‘adada maa Khalaqa fis-samaai, wa Subhaana-Allaah ‘adada maa Khalaqa fil-ardhi, wa Subhaana-Allaah ‘adada maa bayna dhaalika, wa Subhaana-Allaah ‘adada maa Huwa Khaaliq, wa-Allaahu Akbar mithlu dhaalika, wal-HamduliLLaahi mithlu dhaalika, wa laa ilaah illa-Allaaha mithlu dhaalika, wa laa hawla wa laa quwwata illa bi-Allaahi mithlu dhaalika.  (mara 3)



Ifuatayo ni aina ya Tahmiyd (Kumsifu na Kumshukuru Allaah (سبحانه وتعالى). Na kisa chake kinafuatilia kutaja uzito wa thawabu zake:


اللَّهُمَّ لَكَ الْحَمْدُ كَمَا يَنْبَغِى لِجَلالَ وَجْهِكَ وَعَظِيمِ سُلْطَانِكَ

Allaahumma Lakal-Hamdu kamaa yanbaghiy li-Jalaali Waj-hika wa ‘Adhwiymi Sultwaanika


Kutoka kwa ibn 'Umar kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  amesema:

 ((إن عبدًا من عباد الله قال:    يا رب،  لك الحمد كما ينبغي  لجلال وجهك وعظيم سلطانك ،  فعضلت بالملكين فلم  يدريا كيف يكتبانها، فصعدا إلى السماء فقالا يا رب،  إن عبدا قد قال مقالة لا ندري كيف نكتبها،  قال الله - وهو أعلم بما قال عبده :  ماذا قال عبدي؟  قالا يا رب إنه قد قال:  يا رب لك الحمد كما ينبغي   لجلال وجهك  وعظيم سلطانك.  فقال الله لهما: اكتباها كما قال عبدي حتى يلقاني فأجزيه بها))  إبن ماجه

((Mja katika waja wa Allaah alisema: Ewe Mola wangu! Zako wewe tu sifa zote njema Unayestahiki kushukuriwa kama inavyopasa Utukufu Wako na nguvu Zako kubwa kabisa. Malaika wawili walibabaika hawakujua vipi waandike maneno hayo (jinsi alivyomtukuza utukufu wa Mola wake) Wakaenda kwa Allaah wakasema: Ewe Mola wetu! Hakika mja wako kasema aliyoyasema na wala hatujui vipi tuyaandike. Akasema Allaah: Kwani kasema nini mja wangu? (Na Allaah Anajua aliyoyasema mja Wake bila ya malaika kumwelezea) Wakasema amesema: Ewe Mola wangu! Zako Wewe tu sifa zote njema Unayestahiki kushukuriwa kama inavyopasa Utukufu Wako na nguvu Zako kubwa kabisa. Allaah akasema: Yaandikeni kama alivyosema mja Wangu mpaka atakaponikuta (siku ya malipo) basi nitampa jazaa yake kwa hayo (aliyoyasema) )) [Ibn Maajah 2:1249]

Matumizi Ya ‘In Shaa Allaah’ Ndani Ya Du’aa

Shaykh Swaalih Al-Fawzaan*
Imetafsiriwa na ‘Abdun-Naaswir Hikmany

Haifai, pale Muislamu anapomuomba Allaah kusema, “Ee Allaah nisamehe iwapo utapenda!” Pindipo unapoomba kitu kutoka kwa Allaah, mtu asifanye du’aa yake kuwa na shaka katika uwezo wa Allaah, lakini kinyume chake ni lazima awe na uhakika wa dhana njema kwamba Allaah Ataijibu du’aa yake. Imenukuliwa kutoka Hadiyth sahihi iliyosimuliwa na Abu Hurayrah akisema:
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Asiseme mmoja wenu ‘Ee Allaah! Nisamehe iwapo Unapenda; Ee Allaah, kuwa na Rahmah kwangu iwapo Utapenda,’ lakini ni lazima awe na matumaini kwa Allaah yenye uhakika, kwani hakuna mtu anayeweza kumlazimisha Allaah kufanya kitu dhidi ya Uwezo Wake.)) [Imepokewa na Muslim]

“Kuomba kwa Allaah pamoja na yakini” inamaanisha kwamba mtu asimuombe Allaah kwa maneno ya ‘lakini’ au ‘iwapo’ lakini anatakiwa afanye maombi ya uhakika na kutilia mkazo katika jambo hilo. Inakatazwa kutumia maneno kama hayo kwa hoja mbili:
·         Hakuna mtu mwenye nguvu ya kumlazimisha Allaah kufanya kitu Asichokitaka; Anafanya tu kile Anachokitaka. Tofauti na Allaah, waja wanaweza kulazimika kufanya vitu kutokana na hofu na mfano wa hayo.
·         Kufanya maombi katika hali ya kuwa na shaka kwa Uwezo wa Allaah inaonesha udhaifu wa maombi na ukosefu wa hamu ya kuipaita du’aa hiyo jibu; ukosefu wa yakini katika hapa unamaanisha kwamba mtu hana haja ya Allaah.

Katika simulizi nyengine iliyopokewa na Muslim, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anathibitisha kwamba du’aa ifanywe kwa yakini kamilifu, na mtu asisitize moja kwa moja hamu yake (mbele ya Allaah) ndani ya du’aa zake, kwani hakuna baraka iliyo kubwa kwa Allaah itakayomshinda kubariki (juu ya waja Wake), hata kama baraka hii itaonekana kuwa ni kubwa mno mbele ya macho ya wengine. Allaah, Mtukufu, Anasema:
{{Hakika amri Yake anapotaka chochote (kile kitokee) ni kukiambia: ‘Kuwa’, basi mara huwa.}} [Yasiyn: 82]
Hivyo, Muislamu anahitajika kuwa na ufahamu wa kina kuhusiana na masharti ya imani ya kweli na halikadhalika mambo yanayobatilisha tawhiyd, ili kwamba aweze kumuabudu Allaah katika misingi thabiti.


* Imechukuliwa kutoka Kitabu cha Shaykh Swaalih Al-Fawzaan ‘Muongozo Wa  Itikadi Sahihi’ Guide to Muslim Creed, chapa ya mwaka 2005, ukurasa wa 139 -141.

01 Fadhila Za Kumtaja Allaah



 Amesema Allaah سبحانه وتعالى
:{ فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُواْ لِي وَلاَ تَكْفُرُونِ }
“Nitajeni nami nitawataja, na nishukuruni na wala msinikufuru (Suratul Baqaraha 152)
Na akasema:
 { يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّهَ ذِكْراً كَثِيراً}
“Enyi mlioamini mtajeni Mwenyezi Mungu sana” (Suratul Ahzaab 41 )
Akasema tena:
 { وَالذَّاكِرِينَ اللَّهَ كَثِيراً وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْراً عَظِيماً}
“Nawasifu wanaume wanaomtaja Mwenyezi Mungu sana na nawasifu wanawake wanaomtaja, Mwenyezi Mungu   kawaandalia wote hao msamaha na malipo makubwa” (Suratul Ahzaab 35 )
Akasema tena :
{ وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعاً وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالآصَالِ وَلاَ تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ }
“Mtaje Mola wako  moyoni mwako kwa  unyenyekevu  na kwa uwoga, pasina kudhihirisha sauti, mtaje asubuhi  na jioni, nawala usiwe nikatika wenye kughafilika” (Suratul A’raaf 205)
Mtume صلى الله عليه وسلم amesema :
 }  وقال صلى الله عليه وسلم :" مثل الذي يذكر ربه والذي لا يذكر ربه مثل الحي والميت {
{Mfano wa anaemtaja Mola wake na asiyemtaja ni mfano wa alie hai na maiti }
Na akasema Mtume صلى الله عليه وسلم
وقال صلى الله عليه وسلم :" ألا أنبئكم بخير أعمالكم , وأزكاها عند مليككم، وأرفعها في درجاتكم ، وخير لكم من إنفاق الذهب والورق ، وخير لكم من أن تلقوا عدوكم فتضربوا أعناقهم ويضربوا أعناقكم ؟" قالوا بلى .قال : "ذكر الله تعالى
{Hivi niwaambieni khabari  yamatendo yenu bora, na ambayo ni masafi mno, mbele ya Mola wenu, na ambayo ni yajuu mno katika daraja zenu, na ambayo ni bora kwenu kuliko kutoa  dhahabu na fedha, na ambayo ni bora kuliko  kukutana  na adui zenu, mkawapiga shingo zao, nao wakakupigeni shingo zenu?))  Wakasema masahaba; Ndio . Akasema  Mtume صلى الله عليه وسلم  ((Ni kumtaja Mwenyezi Mungu))
وقال صلى الله عليه وسلم :" يقول الله تعالى : أنا عند ظن عبدي بي ، وأنا معه إذا ذكرني ، فإن ذكرني في نفسه ذكرتهُ في نفسي ، وإن ذكرني في ملأ ذكرته في ملأ خير منهم ،وإن تقرب إلى شبراً تقربت إليه ذراعاً ،وإن تقرب إلي ذراعاً تقربت إليه باعاً ، وإن أتاني يمشي أتيتهُ هرولة "
Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Mwenyezi Mungu  anasema “Mimi niko mbele ya dhana ya mja wangu kwangu, akinitaja moyoni nami ninamtaja moyoni  na akinitaja katika  kundi, nami namtaja  katika kundi bora zaidi ya hilo lake, na akijikurubisha kwangu paa moja, basi mimi najikurubisha kwake kiasi cha dhiraa, na akijikurubisha  kwangu kiasi cha dhiraa, basi mimi nitajikurubisha  kwake kiasi chakuyoosha mkono hadi kati ya kifuwa, na akinijia kwa mwendo mdogo basi nami nitamjia kwa mwendo wa kasi. 
وعن عبد الله بن بسرٍ رضي الله عنهُ أن رجلاً قال : يا رسول الله إن شرائع الإسلام قد كثرت علي فأخبرني بشيءٍ أتشبث به. قال :" لا يزال لسانك رطباً من ذكر الله  
Imepokelewa kutoka kwa Abdalla Bin Busr رضى الله عنه   kwamba mtu mmoja alisema :
“Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ibada za dini zimekuwa nyingi kwangu, basi nieleze kitu  ambacho nitaweza  kudumu nacho.   Mtume صلى الله عليه وسلم  akamwambia : Ulimi wako utaendelea kuwa rutuba  (yaani sio ukavu ) kwakumtaja Mwenyezi Mungu  .
وقال صلى الله عليه وسلم:" من قرأ حرفاً من كتاب الله به حسنة ،والحسنة بعشر أمثالها ، لا أقول : {الم } حرف؛ ولكن : ألف حرف ،ولام حرف ،وميم حرف
Na amesema tena Mtume صلى الله عليه وسلم  “Anaesoma harufu moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu  basi anapata thawabu za jema moja na jema ni kwa mema kumi, sisemi kuwa ‘Alif Laam Miim’ ni harufu moja lakini ni kwamba ‘Alif’ peke yake ni harufu moja, na ‘Laam’ ni harufu , na ‘Miim’ ni harufu”
وعن عقبة بن عامر رضي الله عنه قال : خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم ونحن في الصفة فقال :" أيكم يحب أن يغدو كل يوم إلى بطحان أو إلى العقيق فيأتي منه بناقتين كوماوين في غير إثم ولا قطيعة رحم ؟" فقلنا : يا رسول الله نحب ذلك . قال :" أفلا يغدو أحدكم إلى المسجد فيعلم ، أو يقرأ آيتين من كتاب الله عز وجل خير له من ناقتين ، وثلاث خير لهُ من ثلاث ٍ، وأربع خير لهُ من أربع ، ومن أعدادهن من الإبل
Imepokelewa kutoka kwa Uqbah bin Aamir رضى الله عنه   amesema :  ‘Ametoka Mtume wa Mwenyezi Mungu   na sisi tuko sehemu iitwayo Assufah, akasema “Nani kati yenu anapenda aende kila siku sehemu iitwayo But-haan au Aqiq aje na ngamia  wawili walio  nenepa pasi na dhambi wala kukata udugu?”  Wakasema  maswahaba “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tunapenda hivyo’ akasema Mtume صلى الله عليه وسلم  “Hivi haendi (asubuhi ) mmoja wenu msikitini  akajuwa  au akasoma Aya mbili, za kitabu cha Mwenyezi Mungu?    Hizo aya mbili  ni bora kwake kuliko  kupata ngamia wawili, na endapo atasoma aya tatu zitakuwa  ni bora   kwake  kuliko ngamia watatu, na aya nne ni bora kwake kuliko ngamia wanne, na vilevile zaidi ya hapo.  Aya zozote atakazo zisoma  basi ni bora kwake kuliko hisabu  yake kwa ngamia”
وقال صلى الله عليه وسلم:" من قعد مقعداً لك يذكر الله فيه كانت عليه من الله ترة ومن اضطجع مضجعاً لم يذكر الله فيه كانت عليه من الله ترة
Na Anasema Mtume صلى الله عليه وسلم  “Anaekaa kikao chochote  kile asimtaje Mwenyezi Mungu  katika kikao hicho basi ana dhambi kutoka kwa Mwenyezi Mungu,  na anaelala sehemu yeyote ile kisha asimtaje Mwenyezi Mungu   wakati wakuinuka sehemu hiyo basi ana dhambi kwa Mwenyezi Mungu” 
وقال صلى الله عليه وسلم : " ما جلس قوم مجلساً لم يذكروا الله فيه ، ولم يصلوا على نبيهم إلا كان عليهم ترة ، فإن شاء عذبهم وإن شاء غفر لهم
Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Hapana watu wowote  wale, wanaokaa kikao kisha wasimtaje Mwenyezi Mungu humo, wala wasimswalie Mtume wao  ila  watakuwa wana dhambi. Akipenda Atawaadhibu na Akipenda Atawaghufuria.  
وقال صلى الله عليه وسلم :" ما من قوم يقومون من مجلس لا يذكرون الله فيه إلا قاموا عن مثل جيفة حمار وكان لهم حسرة
Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Hapana watu wowote wale  wanaosimama katika kikao walichokaa, kisha wasimtaje  Mwenyezi Mungu  ila watakuwa wanasimama kama  mzoga wa punda, na watakuja juta kwa kutomtaja Mwenyezi Mungu”
Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment