"Al-Mawaddah

"Al-Mawaddah inamaanisha mapenzi na  mahaba na Ar-Rahmah inamaniisha rehma (upole) na huruma - kama ilivyokuwa mtu anamchukuwa mwanamke ama kwa sababu ya mapenzi kwake, au kwa sababu ya mapenzi juu yake au kwa sababu ya upole na huruma juu yake, kwa kumpa mtoto kutokana na yeye..."[iv]
(Ziada: soma chini kuhusu maonyo ya kuchagua mke aliyoyatoa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam).

Na jinsi mke wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Bi Khadiyjah (Radhiya Allaahu 'anha) alivyosimama kwa namna ya pekee kusaidia sana kumliwaza na kumtuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)   wakati Jibriyl ('alayhis-salaam) alipojitokeza kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwa mara ya kwanza katika pango la Hiraa.  Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alirudi kwa Bi Khadiyjah (Radhiya Allaahu 'anha) akiwa na wahyi wa kwanza na huku moyo wake unapiga na kutetemeka kwa nguvu, na akamwambia Bi Khadiyjah:
"Nifunika! Nifunike!"
Kwa hiyo, (Bi Khadijah) akamfunika mpaka hofu yake ilipotokomea, baadaye Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akamuelezea Bi Khadiyjah (Radhiya Allaahu 'anha) kila kitu kilichotokea na akasema
"Naogopa juu ya kutokewa na kitu kibaya"
(Bi Khadiyjah) akamwambia,
"Abadan! WaLlaahi! Allaah hatokuangusha. Unaweka mahusiano mema baina yako na jamaa zako, unawasaidia masikini na fukara, unawahudumia wageni wako kwa ukarimu na unawasaidia wale ambao wamekumbwa na maafa."[v]

Na usisahau kuhusu mama wa waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) pamoja na taathira yake. Hata Maswahaba watukufu walikuwa wanajipatia elimu ya Hadiyth kutoka kwake., na wengi katika Maswahabiyaat (wafuasi wa kike wa Rasuulu-Allaah) walijifunza vitu mbali mbali kuhusu Sharia zilizowahusu wanawake kutoka kwake.

Sina shaka ya kwamba mama yangu- Allaah Amrehemu - alikuwa na taathira makubwa juu yangu, alikuwa ananihimiza nisome, na alikuwa ananisaidia kwa hilo. Allaah Amuongezee thawabu na Amlipe kwa malipo mema kwa yote aliyonifanyia.

Na pia bila shaka, nyumba ambayo ina huruma, upole, upendo na kujali, pamoja na mafundisho mema ya Kiislam itamuathiri mtu. Kwa hiyo atakuwa - ikiwa Allaah atapenda - mwenye kufanikiwa katika mambo yake na katika kitu chochote - ikiwa kutafuta ilmu,biashara, kupata maisha mazuri, au vingine baada ya hivi. Kwahiyo ni Allaah peke Yake ninayemuomba Anipe mafanikio na Atuongoze sote kwenye yale ambayo Anayapenda na Anaridhia. Na Salam na Amani za Allaah zimfikie Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)    na familia yake, Maswahaba zake na wafuasi wake. 


Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment