UKWELI UJITENGA NA UONGO.



JE WAJUA KUWA KUNA MIPANGO MBALIMBALI INAYOFANYWA NA WAHUSIKA ILI KUPOTOSHA UMMA?

*Je kuna binadamu anayeweza kuwa na sifa ya UTUME bila idhini yake ALLAH (Mwenyezi Mungu)????
*Je kuna mwanadamu anayeweza kufanya kazi za kiutume (kuwa nabii) kwa kufundishwa na mtu/ watu?
*J e nani awezaye kuwa MTUME au Nabii na hakupata nguvu hiyo kwa MWENYEZI MUNGU???
Sasa kuna mpango ambao ulianzishwa na watu wenye tama zao ili kuakikisha mwanadamu anapotea juu ya kumpwekesha ALLAH (Mwenyezi Mungu”  Mpango huo ni pamoja na kitengo kilichoanzishwa  kwa wanaume wa thehebu flani hapa duniani ili wao ndio wawe mitume wa Thehebu hilo” Je yaweza kuwa kweli huo Utume wao ni kutokana na Mwenyezi Mungu?? Je wanaume hao wanaofundishwa na wanadamu wenzao “Je wanaweza kuwa mitume wa kweli?? Au ndio wale Mitue wa Uongo?????
Mpango huo ulioanzishwa ulipewa jina la UTUME WA WANAUME yaani  (UNUM-OMNES)
Kiufupi Utume huu ni utume wa naume wote wa thehebu la  Katoliki unaojulikana kwa jina la
  “UNUM OMNES”   madhumuni na majukumu ya Utume huu kwa wanaume wa Kikatoliki ni kujitolea juu ya makanisa yao hapa Duniani. Pia uwahusisha watu wote wenye umri kuanzia miaka 18 jinsia ya kiume tu. Kwa kuwa Utume huu unawahusu wanaume wote Wakatoriki hivyo kila walipo wanaume wakatoriki wana haki ya kuunda umoja wao, Iwe ngazi ya Juuiya ndogo ndogo za Kikiristo , Kigango na Parokia juu ya Utume huu ambao sio Utume wa kutoa kwa Mwenyezi Mungu bali ni utume wa wanadamu ulioundwa ili watakao upokea waachane na mafundisho ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na badala yake washikamane na mafundisho ya Utume utokao kwa wanadamu. Je kwa hali hiyo kuna Utume wa kweli????
MADHUMUNI YA UTUME HUU WA WANADAMU
 *Kuwaunganisha wanaume wakatoriki wote ambao wana nia, moyo wa kulitumikia kanisa ili waweze kufanya kazi hiyoya Kuutangaza Utume wa uongo kwa  waumini wa makanisa.
 *Kuifadhi , Kuimarisha imani ya Kikatoriki iliyo sawa na imani ya Kipagani ya Mungu katika utatu na pia kuendeleza mafundisho hayo ya Kiutume yatokanayo na wanadamu.
*Kuakikisha muumini anashikamana na amri zitokanazo na mwanadamu na wala sio Mwenyezi Mungu  katika shughuli zake zote za kiroho na kimwili.
*Kushirikiana na vyama vingine vya Kitume na mashirika mengine ya Kikatoriki yaliyopo kila kona ya nchi na bara husika.

CHANZO/ HISTORIA YA  UTUME HUU WA UONGO UNAOFANYWA NA WANADAMU NA KUTOKANA NA WANADAMU WALA SIO MWENYEZI MUNGU HAPA DUNIANI.
Utume huu wa wanadamu uliojaa mafundisho yanayowapinga Mitume na Manabii wa Mwenyezi Mungu  ulianzishwa mwaka 890 Hata hivyo Utume huo wa uongo  haukuwa na nguvu sana kutokana na kuwepo kwa Dola ya kiislam hivyo wengi walikuwa wameshikamana na haki. Uliendelea kufahamika kwa uchache kwa kipindi kirefu sana. kisha ulikuja kukua na kufufuliwa mwaka 1922 huko Ulaya  Barani Australia  hadi mwaka 1947 wakati  huo  Wakatoriki waliungana kufanya  jubilee ya miaka 25 na kufanya mkutano maalumu ulioudhuliwa na wajumbe mbalimbali hapa duniani ili katika mkutano huo washauliane  kuunda kamati maalumu ya kuandaa katiba rasmi mwaka 1948 kamati hiyo ilianza kuishughulikia katiba mnamo tarehe 15 hadi 17 August 1950.
Baraza kuu la kwanza la kimataifa la Wanaume Katoliki (International Conci of Catholic Men) lilikuatana huko Vatican “Roma” makao maalumu ya Kiongozi wanaomuita  Baba mtakatifu . Wakati huo Baba mtakatifu PAPA PIO WA XII aliidhinisha Utume huu wa uongo na kuupa jina la “UNUM OMNE” Papa Pio wa xii aliteua utume huu uwe na makao makuu yake Vatikan” Roma” na Utume huu ndiyo chama pekee cha Kitume chenye Makao makuu yake Vatican.
Baadaye Utume huu ulianza kuenezwa sehemu nyingi ulimwenguni hasa Ulaya, Hivyo ilionekana umuhimu wa kueneza Utume huu katika sehemu nyingine na Africa  ikiwa mojawapo. Hivyo umeenezwa mataifa yote , majimbo yote , Parokia zote za Kikatoliki.
KWA UPANDE WA TANZANIA
Mwaka 1985 Utume huu ulianzishwa kwa mara ya kwanza katika Jimbo la keko huko Dar es salaam 1986 mwezi Septemba , Utume ulianzishwa katika jimbo kuu la Dar es salaam , Jitihada zilikuwa zikiendelea kufanyika ili kueneza utume katika majimbo mengine ya Tanzania hadi wanaume wote Wakatoliki watakapohusika kikamiifu na utume wao.
Utume huu umeenea kwa kasi katika majimbo ya  Dar es salaam , Kahama, Tanga, Dodoma, Morogoro , Arusha, Kagera , Same, Mwanza, Tabora, Shinyanga na Songea . Hivyo kwa mwenye akili timamu ajiulize huu ni utume unaotokana Mwenyezi Mungu??
Je kama ni utume unaoundwa na wanadamu huo sio utume wa Uongo???

Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment