IDD MUBARAK WANA DAIMA ANGAZA

Mwezi umeonekana nchi mbalimbali duniani na in Shaa Allaah kesho Ijumaa tarehe 15.06.2018M ni 'Iyd Al-Fitwr.
Daima angaza inawaombea 'Iyd njema yenye furaha na amani.
Taqabbala Allaahu minnaa wa minkum.
Iyyaaka na'buduu. "Wewe tu twakuabudu" . Neno la Kiarabu 'ibaada lina maana ya kutangaza umoja wa Mwenyezi Mungu, pia kumpenda kabisa, kutumainia kabisa, kumwogopa kabisa na kumnyenyekea kabisa. Tena ibada si kusali na kufunga tu, bali kila tendo jema linalofanywa kwa nia ya Kumpendeza Mungu, linakuwa ibada na linampatia mtu thawabu. Kwa kusema "twakuabudu" ambayo ni dhamiri ya wingi, Mwislamu anafundishwa ya kuwa mtu hakai peke yake duniani na ni lazima awe pamoja na wenzake katika mambo yote mema. Pili, mtu anapotaka salama asiwaachie wenziwe kupotea, afanye bidii kuwasuluhisha; kwani nyumba inayozungukwa na nyumba zingine zinazowaka moto haiwezi kuwa salama kwa muda mrefu.
Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment