MSAADA WAKO KATIKA IMANI NI BORA KULIKO FAIDA YA DUNIANI

Asaalam Aleykum Warahmatullah Wabarakatuh 
Ndugu zangu katika Imani ya Hapana Mola anayesitahiki kuabudiwa kwa haki ila ALLAH na Mohammed ni mja wake'''  Sisi kama DAIMA ANGAZA tumependa kushiliki nawe katika hali ya kuakikisha kwa kila namna tunapiga atua nayo si atua nyingine isipokuwa ni hatua ya kuakikisha Uislam unaendelea. Toka alipo zaliwa Mtume wetu (S.A.W) Uislam imekuwa ndiyo dini inayoimiza kusimamisha Uislam na kwa jukumu hilo sisi kama Waislam limebaki kuwa ni jukumu letu kuakikisha kila linalotuhusu katika Uislam tulifanye ili kudumisha udungu wa Kiislam na kuiendeleza dini yetu ya Uislam.

Ndugu zangu katika Imani DAIMA ANGAZA imefanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali kwa kadili ALLAH anavyojalia na kwa siku ya tarehe 16/06/2018 DAIMA ANGAZA ilibahatika kufika eneo moja linalopatikana Mkoa wa KAGERA Wilaya ya MULEBA Kata - MUSHABAGO eneo linalojulikana kama KYANSHENGE huko kulikuwa na Waumini wenzetu ambao kwa kupata taabu sana ya kukosa Msikiti waliamua kujipinda tena kwa hali ngumu na kuweka Msikiti wa Makuti ambao hata sisi wanaDAIMA ANGAZA tulijaliwa kusali na Swala ya IDD na Swalatil Jumaa mahali hapo . Miongoni mwa hali tuliyokutana nayo ni hali ya kusikitisha maana wanadhiki lakini pamoja na dhiki zao hawajakubali kuuacha Uislam. 
Ndugu zangu katika Imani sisi kama DAIMA ANGAZA tunakuomba uungane na sisi katika kujitolea kwa chochote kile ulichojaaliwa na ALLAH atakulipa ili tuweze kuwezesha uwepo wa Msikiti kwa Waumini wa pale maana wanapata sana taabu na changamoto bado zipo maana mwalimu wa madrasa hayupo kiukweli ni mtihani mkubwa. 
Mchango wako tuma katika akaunti hii O765435802 (Sultan Abdul Mabege) 

                            HIZI NI PICHA ZA ENEO HUSIKA NA HALI YA MSIKITI ILIVYO                   
Huu ndio Msikiti wa Waumini
#Kulia ni Muumini wa Msiktini hapo Kharid Hussen na #Kushoto ni Mwana DAIMA ANGAZA Sultan ambaye alijaliwa kufika maeneo hayo ya KYANSHENGE -MUSHABAGO MULEBA KAGERA TANZANIA.

Ukweli Ndugu zangu katika Imani hali ya Uislam huku Vijijini ni hali ngumu tunaomba sana tena sana tuungane katika kudumisha Uislam na kuakikisha tunaendeleza jihadi hii ya kuusimamisha Uislam.


Haya ni maji ambayo yanapatika atua kidogo toka ulipo Msikiti ni kama hatua 10.....Maji haya wanayatumia kama maji ya kuwawezesha kufinyaga udongo na kuweza kupachakia nyufa ila muda mwingine maji hayo utumika kustanjia ama katika shughuli nyinginezo. Hata maji ya kupatia UDHU ni mtihani kwa kweli. Ila pamoja na dhiki hiyo bado waumini wanatafuta faraja ya ALLAH.

# UISLAM ni dini ya TAWHIDI hivyo aijali mali wala rangi wala kabila wala haishikamani na Siasa isipokuwa ni Muumini kujinyenyekeza Kwa ALLAH (S.W) ili apate kurehemiwa. Huu ni Usafili wa Ustadhi anaotumia kuwasili Msikitini hapo ili aungane na Waumini wenzake katika suala zima la Uislam.

Huu ni Msikiti wa Waumini wa KYANSHENGE iliyopo maeneo ya RUITA wilaya ya MULEBA Mkoa KAGERA.

Hali ndo hii katika eneo hilo.


Ndugu zangu Waislam hali ndo hii na ukweli ni kwamba kila kitu utachojaliwa kutoa kwa ajili ya ALLAH na yeye ndiye mwenye kujua mwenye kuona nia ya Mwenye kutoa.
Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment