Kama ilivyo kawaida ya ANGAZA ni kuakikisha inangaza na wewe katika kweli hili tuwe huru maana imeandikwa kuwa UKWELI WA MUNGU HAUTAFICHIKA KAMWE.
25 Swafar 1438 H | |
Jiunge Upokee Jarida La AlhidaayaUser login |
Nani Aliandika Biblia?
SWALI:
ASALAM ALEYKUM
Ndugu zangu waislam, naombeni kuuliza swali, eti nani aliandika biblia?
JIBU:
AlhamduliLlaah
- Himdi Na Sifa Zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa
walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya
Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Mwanzo
inatakiwa ifahamike kuwa Biblia si kitabu kinachotoka kwa Mwenyezi
Mungu. Vitabu vitukufu vilivyoteremshwa na Allaah Aliyetukuka ni Suhuf
(nyaraka) za Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam), Taurati ya Nabii
Muusa (‘Alayhis Salaam), Zaburi ya Nabii Daawuud (‘Alayhis Salaam),
Injili ya Nabii ‘Iysa (‘Alayhis Salaam) na Qur-aan ya Nabii Muhammad
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Biblia ni neno
lililotokana na neno la Kigiriki Biblios lenye maana ya mkusanyiko wa
vitabu vingi. Biblia yenyewe inatuhakikishia kuwa kuna mikono ya
waandishi iliyoingia katika kutunga walichotaka ndani yake. Hii ni kwa
mujibu wa Yeremia 8: 8: “Mnawezaje kusema: ‘Sisi tuna hekima, sisi
tunayo sheria ya Mwenyezi-Mungu,’ hali waandishi wa sheria wameipotosha
sheria yangu?”
Kulingana
na wanazuoni wa Biblia, hata utunzi wa vitabu vya Agano la Kale na
Anaajiyl (wingi wa Injili) zenyewe zina shaka na utata.
Taurati
Vitabu vitano vya kwanza vya Biblia (Pentateuch - Mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Sheria.) kiada zinanasibishwa na Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam), hata hivyo, zipo aya nyingi sana katika vitabu hivi ambazo zinaashiria kuwa haiwezekani kwa Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam) kuwa aliandika kila kitu ndani yake. Kwa mfano, Kumbukumbu la Sheria 34: 5 – 8 inayosema: “Basi Mose (yaani Musa) mtumishi wa Mwenyezi Mungu akafariki huko nchini Moabu kulingana na neno la Mwenyezi Mungu alilosema. Mwenyezi Mungu akamzika katika bonde la Moabu, mkabala wa mji wa Beth-peori; lakini mpaka leo, hakuna mtu ajuaye mahali alipozikwa. Mose alikuwa na umri wa miaka mia moja na ishirini alipofariki; macho yake yalikuwa hayajafifia, na alikuwa timamu na mwenye nguvu. Waisraeli waliomboleza kifo chake
kwa muda wa siku thelathini kwenye nchi tambarare ya Moabu. Kisha siku
za matanga na maombolezo ya kifo chake zikaisha”. Ni dhahiri kuwa mtu
mwengine ndiye aliyeandika aya hizi kuhusu kifo cha Nabii Muusa
(‘Alayhis Salaam).
Katika
kiambatisho cha RSV kilichopatiwa anwani “Books of the Bible – Vitabu
vya Biblia”, yafuatayo yameandikwa kuhusu utunzi wa zaidi ya thuluthi ya
vitabu vilivyobakia katika Agano la Kale:
Hata
Zaburi nayo ina matatizo kwani katika Sura ya 72: 20 inasema: “Mwisho
wa sala za Daudi mwana wa Yese”. Lakini Zaburi inaendelea hadi Sura ya
150. Je, ni nani aliyeandika Zaburi 73 – 150? Sura ya 73 ina kichwa cha
habari: Haki itatawala (Zaburi ya Asafu). Je, huyu Asafu ni nani?
Apocrypha
Zaidi ya nusu ya Wakristo duniani ni Wakatoliki. Nakala yao
ya Biblia ilichapishwa mwaka wa 1582 kutoka kwa Jerome’s Latin Vulgate
(Biblia ya Kikatoliki ya Jerome), na kunakiliwa tena hapo Douay mwaka wa 1609. Agano la Kale la Roman Catholic Version (RCV – Nakala ya Kikatoliki) ina vitabu saba zaidi kuliko KJV inayotambulika na Waprotestanti. Vitabu hivi vya ziada zinajulikana kama
Apocrypha (yaani utunzi wenye shaka) na zilitolewa kutoka katika Biblia
katika mwaka wa 1611 na wanazuoni wa Biblia wa Kiprotestanti.
Anaajiyl
Aramai
ilikuwa ndio lugha iliyokuwa ikitumiwa na Mayahudi huko Palestina. Kwa
hiyo, inaaminika kuwa Yesu na wanafunzi wake walizungumza na kufundisha
kwa Kiaramai. “Simulizi za kwanza ya mdomo za matendo ya Yesu na kauli
zake bila shaka zilisambaa kwa Kiaramai. Hata hivyo, Injili nne
ziliandikwa kwa ukamilifu wake kwa maneno mengine, Kiyunani ya kawaida,
lugha iliyokuwa ikitumika katika dunia ya Kistaarabu ya Mediterania, ili
kutumikia wengi katika Kanisa, ambayo ilikuwa ni ya Kiyunani (wenye
kuzungumza Kigriki) badala ya Kipalestina. Mabaki ya Kiaramai yalikuwepo
katika Anaajiyl za Kiyunani. Kwa mfano, katika Marko 5: 41,
“Kisha akamshika mkono, akamwambia, ‘Tal’itha cu’mi’, maana yake,
‘Msichana mdogo, nakuambia amka’”. Pia Marko 15: 34: “Saa tisa alasiri
Yesu akalia kwa sauti kubwa, ‘Eloi, Eloi, lama sabachthani?’ maana yake,
‘Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?’” (Encyclopedia Americana, Mj. 3, uk. 654).
Injili
ya Marko katika Agano Jipya, japokuwa inachukuliwa na wanazuoni wa
Kanisa kuwa ndio kongwe kabisa kati ya Anaajiyl, haikuandikwa na
mwanafunzi wa Yesu. Wamehitimisha wanazuoni wa Biblia, kutegemea na
dalili zinazopatikana katika Injili, kuwa Marko mwenyewe hakuwa
mwanafunzi wa Yesu. Zaidi ya hayo, kulingana na wao, haijulikani kamwe
huyu Marko alikuwa nani kwa uhakika. Mwandishi wa kale wa Kikristo,
Eusebius (325 BI), alipokea kuwa mtunzi mwengine wa zamani, Papias (130
BI), alikuwa wa kwanza kuinasibisha Injili kwa John Mark (Yohana Marko),
mwandani na mfuasi wa Paul (Paulo). Wengine wametoa rai kuwa huenda
alikuwa mwandishi wa Petro na ilhali wengine wanaona kuwa huenda alikuwa
mtu mwengine kabisa.
Hiyo
ndiyo hali ya Injili nyingine. Japokuwa Mathayo, Luka na Yohana
yalikuwa majina ya wanafunzi wa Yesu, waandishi wa Injili hizo waliokuwa
na majina ya wanafunzi hao mashuhuri, lakini ni watu wengine ndio
waliotumia majina yao ili maelezo yao yapate kusadikika. Kwa hakika,
Injili zote zilisambaa hapo awali bila majina. Baadaye majina yenye
kuaminika yalipatiwa kama watunzi wa Injili hizo na watu wasiojulikana
katika kanisa za awali.
Na Allaah Anajua zaidi
»
|
Yanayohusiana
FeatureZingatioNyumba Ya Akhera Umeshaijenga?
Miongoni
mwa nguzo za iymaan ni kuamini kwamba kuna hesabu Siku ya Qiyaamah.
Hesabu ambayo itamtambua kwamba ni mtu wa Peponi ama ni motoni. Mola
Atujaalie kuwa miongoni mwa watu wa Peponi, Aamiyn.
|
|
0 comments:
Post a Comment