HADITY AL-QUDSIY HADIYTH YA 42.

Hadiyth La Wiki

Hadiyth Al-Qudsiy Hadiyth Ya 42: Watu Wa Jannah Watapata Ridhaa Ya Allaah

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ اللَّهَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى يَقُولُ لِأَهْلِ الْجَنَّةِ: يَا أَهْلَ الْجَنَّةِ!  فَيَقُولُونَ لَبَّيْكَ رَبَّنَا وَسَعْدَيْكَ،   فَيَقُولُ: هَلْ رَضِيتُمْ؟  فَيَقُولُونَ وَمَا لَنَا لَا نَرْضَى وَقَدْ أَعْطَيْتَنَا مَا لَمْ تُعْطِ أَحَدًا مِنْ خَلْقِكَ،   فَيَقُولُ:  أَنَا أُعْطِيكُمْ أَفْضَلَ مِنْ ذَلِكَ،   قَالُوا: يَا رَبِّ وَأَيُّ شَيْءٍ أَفْضَلُ مِنْ ذَلِكَ؟  فَيَقُولُ: أُحِلُّ عَلَيْكُمْ رِضْوَانِي فَلَا أَسْخَطُ عَلَيْكُمْ بَعْدَهُ أَبَدًا)) البخاري،  مسلم و الترمذي
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Atawaambia watu wa Jannah: Enyi watu wa Jannah! Watasema: Labeka Rabb wetu tuko chini ya amri Yako na kheri zote zimo katika Mikono Yako. Kisha Atasema: Je, mmeridhika?  Watasema: Vipi tusiridhike na hali Umetupa ambayo Hukumpa yeyote mwengine katika viumbe Vyako? Kisha Atasema:  Nitakupeni kilicho bora kuliko hayo. Watasema: Ee Rabb, ni kipi kilicho bora kuliko haya? Atasema: Nitafanya ridhaa (mapenzi) Yangu iwateremkie na baada ya hapo Sitoghadhibika nanyi tena abadan) [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhy]

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ -Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada:Kutawasali Kwa Du'aa Ya Nabiy Yuwnus

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ
Wewe Pekee Tunakuabudu
Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

Tawassul Zinazokubalika Katika Shariy’ah

Kutawasali Kwa Du'aa Ya Nabiy Yuwnus ('Alayhis-Salaam)

Du'aa ya Nabiy Yuwnus ('Alayhis-Salaam) ni sababu mojawapo kubwa ya kuitikiwa du’aa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Nabiy Yuwnus ('Alayhis-Salaam) baada ya kuwalingania watu wake katika Tawhiyd wakakanusha, aliwakimbia bila ya kupata idhini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) hivyo akamkosea Rabb Wake. Baada ya kutupwa baharini kutoka katika jahazi aliyoipanda kwa ajili ya kukimbia mbali, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akamuamrisha nyangumi ammeze bila ya kumla nyama yake au kumvunja mifupa yake. Akabakia tumboni mwa nyangumi kwa masiku kadhaa, akawa anaomba du’aa hiyo ya kujirudi kwa Rabb Wake.
Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:
 وَذَا النُّونِ إِذ ذَّهَبَ مُغَاضِبًا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقْدِرَ عَلَيْهِ فَنَادَىٰ فِي الظُّلُمَاتِ أَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٧﴾
Na Dhan-Nuwn (Yuwnus) alipoondoka akiwa ameghadhibika, akadhani kwamba Hatutamdhikisha; akaita katika kiza kwamba: “Hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Utakasifu ni Wako, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.” [Al-Anbiyaa: 87]

Basi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akamtakabalia:
فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْغَمِّ ۚ وَكَذَٰلِكَ نُنجِي الْمُؤْمِنِينَ ﴿٨٨﴾
Basi Tukamuitikia na Tukamuokoa kutokana na ghamu. Na hivyo ndivyo Tuwaokoavyo Waumini.  [Al-Anbiyaa: 88]

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akathibitisha kwamba du’aa hiyo aliyoiomba Nabiy Yuwnus ('Alayhis-Salaam) ni du’aa inayosababisha kutakabaliwa du’aa:
عَنْ سَعْدٍ بن أبي وقاص (رضي الله عنه)  قَالَ:  قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ: ((دَعْوَةُ ذِي النُّونِ إِذْ دَعَا وَهُوَ فِي بَطْنِ الْحُوتِ: "لاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنْتُ مِنْ الظَّالِمِينَ" فَإِنَّهُ لَمْ يَدْعُ بِهَا رَجُلٌ مُسْلِمٌ فِي شَيْءٍ قَطُّ إِلاَّ اسْتَجَابَ اللَّهُ لَهُ))
Kutoka kwa Sa’d bin Abi Waqaasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Du’aa ya Dhan-Nuwn (Nabiy Yuwnus 'Alayhis Salaam) alipoomba alipokuwa katika tumbo la nyangumi:
Laa ilaaha illa Anta Subhaanaka inniy kuntu minadhw-dhwaalimiyn
basi hakika hakuna Muislamu aombaye kwayo kitu chochote kile ila Allaah Atamuitikia)) [Swahiyh At-Tirmidhiy (3505), Swahiyh Al-Jaami’ (3383), Takhriyj Al-Mishkaat Al-Maswaabiyh (2232), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (1744)]

Bila ya shaka du’aa ya Nabiy Yuwnus ('Alayhis-Salaam) inastahiki kuwa ni wasiylah ya kutakabaliwa  du’aa kwa sababu du’aa hiyo imegawanyika katika sehemu tatu:
1. Kumpwekesha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
 لاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ
Hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Wewe.

Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema: “(Nabiy Yuwnus ‘Alayhis-Salaam) Amekiri Tawhiyd ya Uluwhiyyah ambayo inahusiana na aina mojawapo ya du’aa (Du’aa ya ‘ibaadah) kwa sababu ‘Ilaah’ Ndiye Mwenye kustahiki kuombwa aina zote mbili za du’aa;  du’aa ya ‘ibaadah na du’aa ya mas-alah (jambo). Naye Ndiye Allaah Hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye.” [Kuulizwa kwake Shaykh kuhusu du’aa ya Dhan-Nuwn]

2. Kumsabbih (kumtakasa) Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
سُبْحَانَكَ
Utakasifu ni Wako.

3. Kukiri madhambi
إِنِّي كُنْتُ مِنْ الظَّالِمِينَ
 Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.

Akasema tena Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: “Kuhusu kauli yake: “Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu” Inahusiana na kukiri kwake dhambi, na hivyo ni kuomba maghfirah.”

Na Istighfaar (kuomba maghfirah) kuna faida tele kwa dalili kadhaa.
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)
اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا ﴿١٠﴾
Ombeni maghfirah kwa Rabb wenu; hakika Yeye ni Mwingi mno wa kughufuria.

يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا ﴿١١﴾
Atakutumieni mvua kutoka mbinguni, tele ya kuendelea.

وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَارًا ﴿١٢﴾
Na Atakuongezeeni mali na wana, na Atakupeni mabustani na Atakupeni mito. [Nuwh: 10-12]

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ -Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada:Kutawasali Kwa Du'aa Ya Nabiy Yuwnus

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ
Wewe Pekee Tunakuabudu
Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

Tawassul Zinazokubalika Katika Shariy’ah

Kutawasali Kwa Du'aa Ya Nabiy Yuwnus ('Alayhis-Salaam)

Du'aa ya Nabiy Yuwnus ('Alayhis-Salaam) ni sababu mojawapo kubwa ya kuitikiwa du’aa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Nabiy Yuwnus ('Alayhis-Salaam) baada ya kuwalingania watu wake katika Tawhiyd wakakanusha, aliwakimbia bila ya kupata idhini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) hivyo akamkosea Rabb Wake. Baada ya kutupwa baharini kutoka katika jahazi aliyoipanda kwa ajili ya kukimbia mbali, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akamuamrisha nyangumi ammeze bila ya kumla nyama yake au kumvunja mifupa yake. Akabakia tumboni mwa nyangumi kwa masiku kadhaa, akawa anaomba du’aa hiyo ya kujirudi kwa Rabb Wake.
Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:
 وَذَا النُّونِ إِذ ذَّهَبَ مُغَاضِبًا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقْدِرَ عَلَيْهِ فَنَادَىٰ فِي الظُّلُمَاتِ أَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٧﴾
Na Dhan-Nuwn (Yuwnus) alipoondoka akiwa ameghadhibika, akadhani kwamba Hatutamdhikisha; akaita katika kiza kwamba: “Hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Utakasifu ni Wako, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.” [Al-Anbiyaa: 87]

Basi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akamtakabalia:
فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْغَمِّ ۚ وَكَذَٰلِكَ نُنجِي الْمُؤْمِنِينَ ﴿٨٨﴾
Basi Tukamuitikia na Tukamuokoa kutokana na ghamu. Na hivyo ndivyo Tuwaokoavyo Waumini.  [Al-Anbiyaa: 88]

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akathibitisha kwamba du’aa hiyo aliyoiomba Nabiy Yuwnus ('Alayhis-Salaam) ni du’aa inayosababisha kutakabaliwa du’aa:
عَنْ سَعْدٍ بن أبي وقاص (رضي الله عنه)  قَالَ:  قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ: ((دَعْوَةُ ذِي النُّونِ إِذْ دَعَا وَهُوَ فِي بَطْنِ الْحُوتِ: "لاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنْتُ مِنْ الظَّالِمِينَ" فَإِنَّهُ لَمْ يَدْعُ بِهَا رَجُلٌ مُسْلِمٌ فِي شَيْءٍ قَطُّ إِلاَّ اسْتَجَابَ اللَّهُ لَهُ))
Kutoka kwa Sa’d bin Abi Waqaasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Du’aa ya Dhan-Nuwn (Nabiy Yuwnus 'Alayhis Salaam) alipoomba alipokuwa katika tumbo la nyangumi:
Laa ilaaha illa Anta Subhaanaka inniy kuntu minadhw-dhwaalimiyn
basi hakika hakuna Muislamu aombaye kwayo kitu chochote kile ila Allaah Atamuitikia)) [Swahiyh At-Tirmidhiy (3505), Swahiyh Al-Jaami’ (3383), Takhriyj Al-Mishkaat Al-Maswaabiyh (2232), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (1744)]

Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment