PAULO
AU YESU? IMANI AU MATENDO?
Hebu yazingatie Mahubiri ya Yesu aliyotoa juu ya Mlima wa Zaituni:
Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua
torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana,
amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja
ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. Basi mtu ye yote atakayevunja amri
moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa
katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo
ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu
isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme
wa mbinguni.
Mathayo 5.17-20
Mnamo mahubiri ya Mlima wa Zaituni ndio yanapatikana mafunzo makubwa
ya Yesu Kristo. Tunaweza kusema kuwa humu, khasa, ndio umo Ukristo;
yaani ikiwa tunaamini ya kuwa Yesu ndiye Katika kifungu cha maneno hayo
tuliyoyanukulu ya Yesu tunaona ya kuwa ni muhali mtu kuingia katika ufalme wa
mbinguni, yaani Peponi, mpaka haki ya mtu izidi ile ya waandishi na Mafarisayo.
Yaani wema uutendao uzidi ule wa wanazuoni wa Kiyahudi. Ni nini hiyo haki
ya waandishi na Mafarisayo? Ni kuifuata sharia ya Taurati neno kwa neno,
na pia waliofunza manabii wengineo. Ndio maana Yesu akasema: "Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii, sikuja
kutangua, bali kutimiliza." Kazi yake haikuwa kutengua sharia ya Taurati na
kuleta kitu kingine cha kutengua au kugonganisha na mafunzo ya sharia ya
Mwenyezi Mungu na Mitume wake, bali kaja yeye kutimiliza kwa kuwafunza Mayahudi
umuhimu wa mambo ya kiroho katika sharia. Kutii madhaahiri ya sharia tu na
kuwacha undani wake, uchamngu, hakutoshi. Mwenyezi Mungu atiiwe kwa dhaahiri na
kwa siri. Yesu alishikilia sana kufundisha na kutenda, aliposema:
"Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi
zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa
mbinguni; bali atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika
ufalme wa mbinguni."
Katika amri za Taurati ni kama hii iliyomo katika Biblia:
Katika amri za Taurati ni kama hii iliyomo katika Biblia:
Na
nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini
hacheui, yeye ni najisi kwenu. Msile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao;
hao ni najisi kwenu.
Mambo ya Walawi 11.7-8
Kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Msile damu ya
mnyama wa aina yo yote; kwa kuwa uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu
yake; atakayeila awaye yote atakatiliwa mbali. Tena kila mtu atakeyekula
nyamafu, au nyama aliyeraruliwa na wanyama, kama ni mzalia, kama ni mgeni,
atafua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni; ndipo
atakapokuwa safi.
Walawi 17.14-15
Hizo ni amri ziliomo katika Taurati, sharia ya Mungu, ambayo Yesu
amesema kama ilivyo katika Injili ya Mathayo kuwa mwenye kuivunja ndogo yao na
akawafundisha watu hivyo basi ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa
mbinguni. Na kuvunja hayo khasa ndio Paulo kafundisha. Msikieni:
Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila
kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri; maana Dunia ni mali ya Bwana na
vyote viijazavyo.
1 Wakorintho 10.25-26
Mnamwona Paulo anavyobomoa sharia ya Taurati waliyoifwata
Manabii wote, hata Yesu na wanafunzi wake thenashara, ya kuwa kuna vyakula
vilivyo halali na kuna vingine ni najisi, haramu kuliwa, kama nguruwe, vya
kunyongwa na damu? Yesu kafunza nini, na Paulo anafunza nini!
Katika waraka wake aliowapelekea Wagalatia Paulo anasema:
Katika waraka wake aliowapelekea Wagalatia Paulo anasema:
Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki
kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema, Maana sisi kwa Roho
tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani. Maana katika Kristo Yesu
kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa
upendo.
Wagalatia 5.4-6
Kwa kauli moja Paulo ameitengua sharia yote. Yesu kasema nini juu ya
Mlima wa Zaituni na Paulo anasema nini katika barua yake kwa Wagalatia?
Yesu alifuata sharia ya Mwenyezi Mungu na aliihishimu na akaahidi kuwa yeye
hatoitengua kabisa, ila ataitimiza. Paulo anaibeza sharia na kuiona kuwa ni
laana. Yesu akila kilicho halalishwa na Mungu, na alikiepuka kilicho harimishwa
na Mungu. Paulo anatwambia tule kila kiuzwacho sokoni bila ya kujali dhamiri
yetu. Yesu na Manabii wote tangu Nabii Ibrahim walitahiriwa kwa kufuata
amri ya Mungu kama isemavyo Biblia:
Mungu
akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi
vyao baada yako. Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na
wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa.
Mwanzo 17.9-10
Paulo mjuaji, anasema kumpinga Mungu:
Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa,
bali kiumbe kipya.
Wagalatia 6.15
Katika barua yake aliyowapelekea Warumi ndio kabisa Paulo anaiangamiza
sharia ya Mungu na kufanya vitendo kuwa havina maana yo yote.Chenye maana peke
yake ni imani tu.
Basi, twaona ya kuwa wanadamu huhesabiwa haki kwa
imani pasipo matendo ya sheria.
Warumi 3.28
Kwa Paulo kuamini kuwa Yesu kafa msalabani na damu yake kuwa ni fidia
kwa dhambi zetu ndio kwenye maana, sio kufuata sharia wala vitendo. Kwake
yeye ile Taurati, ambayo Yesu mwenyewe hakuja kuitengua bali kaja makusudi
kuitimiza, ni kifungo na pingamizi. Anawaambia Warumi:
Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali
ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika
hali ya zamani, ya andiko.
Warumi 7.6
Paulo anaiona Taurati ni kifungo, pingamizi, bali ni laana. Hayo sio
maoni ya Yesu ambaye amesema: "Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi
moja wala nukta moja ya torati haitaondoka." Je, kwa kuingia Paulo katika
umoja wa Kikristo ndio tusema mbingu na nchi zimeondoka? Au kwa
kutundikwa Yesu msalabani (ikiwa kweli katundikwa) ndio tuseme mbingu na nchi
zimeondoka? Mbona watu wameyasahau upesi maneno ya Yesu mwenyewe, na
kuyasikiliza ya Paulo? Kwa sababu yanakubaliana na matamanio yao?
Mafunzo ya Paulo yalileta mzozano na ubishi mkubwa tangu pale mwanzo katika historia ya Kanisa baina ya kikundi chake cha Wakristo waliomfuata kutoka upagani, na wale Wakristo wa asli ya Kiyahudi. Wao walipinga moja kwa moja ile shauri ya kwenda kupelekewa mafunzo ya Ukristo mataifa waliokuwa hawakutahiriwa, wala hawaikubali sharia ya Taurati. Baadhi ya wanafunzi wa Yesu walikuwa hawakubali hata kula nao wale "wasiotahiriwa". Wao walikuwa wanajua vyema kuwa Yesu aliwakataza wasiende kuwahubiria mataifa mengine isipokuwa Mayahudi tu, kwani ni wao ndio walikuwa wanaamini Mungu Mmoja na wao ndio wakiifuata sharia ya Mungu. Mwishoe ulifanywa mkutano na yakawapo baadhi ya masikilizano kuwa yafaa kuhubiriwa Ukristo kwa mataifa yasiokuwa ya Kiyahudu, na wao wasilazimishwe kubeba mizigo mizito katika dini kama vile wenye asli ya Kiyahudi. Walitumwa Paulo na Barnaba kuwaendea hao mataifa, nao ni Wazungu wa Kirumi na Kigiriki, na wakachukua barua iliomalizikia maneno haya muhimu:

Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi,
tusiwatwike mzigo ila hayo yaliyo lazima, yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa
sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa na uasherati.
Mkijizuia na hayo mtafanya vema. Wasalamu.
Matendo 15.28-29
Nyama zilizosongolewa, yaani nyama za kunyonga, zisiochinjwa.
Yazingatieni haya si maamrisho ya Yesu, lakini ni masikilizano baina akina
Paulo na wanafunzi wake Yesu,(kwa ridhaa ya Roho Mtakatifu) baada ya kuwa Yesu
mwenyewe hayupo tena. Ikiwa hayo ndiyo waliokubaliana ilikuwaje Paulo tena
kuwaandikia Wakorintho: "Kila
kitu kiuzwacho sokoni kuleni bila ya kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri"? Lakini
Paulo ni Paulo.
Mtakatifu Paulo anadai kuwa yeye aliteuliwa makhususi kuwa ni mtume wa Yesu katika ufunuo (Wahyi), na kuwa bado yeye anaendelea kupata amri moja kwa moja kutokana na mwenyewe Bwana Yesu, ijapokuwa amri hizo na mafunzo hayo yanapingana kabisa na yale waliyoyapata wale wanafunzi wake Yesu waliokuwa naye mwenyewe alipokuwa hai. Yeye Paulo hakupata kuonana na Yesu, bali yeye alikuwa ni mpinzani mkubwa wa Ukristo na akawa ni sababu ya kuteswa na kuuwawa Wakristo kadhaa wa kadhaa, mmoja wao ni Mtakatifu Stefano, shahidi wa mwanzo katika Wakristo. Paulo alikuwa na asli ya Kiyahudi, na dini yake rasmi ilikuwa ya Kiyahudi. Kwa kuwa alizaliwa nje ya Palastina katika mamlaka ya Kirumi alikuwa na uraia kamili wa Kirumi, na huko alipata fursa ya kusoma ilimu na falsafa za Kiyunani. Mazingara yake yote ya Kigiriki na Kirumi yalikuwa ya kikafiri, kipagani. Kwani Magiriki na Warumi walikuwa washirikina wenye kuamini chungu ya miungu, kama ilivyokuwa ada ya karibu mataifa yote ya wakati ule isipokuwa Mayahudi. Yalipozuka mafunzo ya Yesu Kristo, ambayo kwa asili yake hayakuwa ila ni kuendeleza ile ile imani ya Kiyahudi ya Mungu Mmoja na kufuata sharia ya Taurati na kuongeza uchamngu, na ikawa mafunzo hayo yanaendelea juu ya kupingwa, Paulo aliona anaweza kuipa nguvu hiyo dini au kwa hakika madhehebu mapya kwa kuwatia wale Warumi na Magiriki kwa kuchanganya imani zao na falsafa zao pamoja na imani ya Kiyahudi. Mayahudi wanaamini Mungu Mmoja, ndio. Ukristo unaamini Mungu Mmoja. Magiriki na Warumi wanaamini miungu mingi, si chini ya watatu, ndio na Ukristo nao unaamini hivyo. Jee, si pana mgongano hapo? La, katika Ukristo imani ni ya Mungu Mmoja katika Utatu Mtakatifu: Mungu Mmoja, mwenye nafsi tatu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Mapagani wa Kigiriki na Kirumi wakiamini mungu aliyekufa, akafufuka na akapaa mbinguni. Hilo si kitu wanaweza kuendelea na imani hiyo katika Ukristo. Wazungu magovi hawataki kutahiriwa. Hapana kitu, kutahiriwa si kitu wala kutotahiriwa. Hoja ipatikane tohara ya roho. Wazungu wamezoea kula kila kitu, nguruwe, damu, kilichochinjwa na kisichochinjwa. Hilo si tatizo, mtaendelea vivyo hivyo, kwani dhambi ni kitokacho mdomoni, sio kiingiacho. Kuleni kila kiuzwacho sokoni. Hapana halali wala haramu. Huo ndio Ukristo mpya wa Paulo, na hiyo ndio Thiolojia yake ambayo, inasikitisha Wakristo wameifuata, wakayaacha mafunzo mepesi na yaliyonyooka ya mwenyewe Yesu Kristo.
Hayo ni maji makuu, letu sisi ni kuangalia yaliyomo ndani ya Biblia Takatifu. Tuiache hiyo iseme. Khabari za kugeuka Paulo akaacha kumpinga Yesu, na badala yake akawa mfuasi wake zinasimuliwa pahala patatu katika Matendo ya Mitume katika Agano Jipya la Biblia. Na katika zote mara tatu kisa hicho kinakhitalifiana katika mambo muhimu. Kwanza tunasoma katika Sura ya 9 mstari wa 3 mpaka wa 7:

Hata (Paulo) alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia
Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini,
akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, (yaani Paulo) mbona waniudhi?
Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi
wewe. Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo
kutenda. Na wale waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, wakiisikia
sauti, wasione mtu.
Matendo 9.3-7
Katika maelezo hayo hapo ni mwandikaji anasimulia. Yapo mambo mane
lazima tuyazingatie vizuri katika maelezo hayo:
- Mwangaza ambao Paulo ulimwangaza. Haikusemwa kuwa wengine waliuona mwangaza ule au la, lakini waliisikia sauti.
- Ni Paulo ambaye "akaanguka chini."
- Yeye na wale watu waliokuwa pamoja naye waliisikia sauti, lakini hawakumwona mtu.
- Sauti ya Yesu ilimuamuru "aingie mjini, naye ataambiwa yampasayo kutenda." Hapo hakuambiwa nini la kutenda.
Katika Biblia hiyo hiyo, katika kitabu hicho hicho cha Matendo ya Mitume, sura 22, mstari wa 6 mpaka wa 10
ipo ncha ya pili ya hadithi kusimulia tukio lile lile. Msimulizi hapa ni Paulo
mwenyewe:
Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski,
wakati wa adhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote.
Nikaanguka nchi (yaani chini), nikasikia sauti ikiniambia, Sauli, Sauli, mbona
unaniudhi? Nikajibu, Wewe u nani, Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu
Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi. Na wale waliokuwa pamoja nami waliiona
ile nuru, lakini hawakuisikia ile sauti ya yule aliyesema nami. Nikasema,
Nifanye nini, Bwana? Bwana akaniambia, Simama, uingie Dameski, na huko
utaambiwa habari za mambo yote yaliyoamriwa uyafanye.
Matendo 22.6-10
Ncha hii yakubaliana na ile ya mwanzo katika mambo haya:
- Aliyeanguka chini ni Paulo na sio wale waliokuwa pamoja naye.
- Aliloambiwa Paulo ni kuingia mjini na huko ndiko atakoambiwa nini la kulifanya.
Ncha hii lakini inakosana na ile ya kwanza kuwa ya kwanza yasema ya
kuwa wale waliokuwa naye "wakasimama
kimya, wakisikia sauti, lakini haikusema kuwa waliona nuru.
Katika ncha hii ya pili twaambiwa: waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia ile sauti.
Ncha ya tatu ya tukio hilo hilo muhimu kabisa katika historia ya Ukristo inaelezwa katika maneno yake mwenyewe Paulo vile vile kama inavyosimuliwa katika kitabu kile kile cha Matendo ya Mitume sura ya 26 mstari wa 12 mpaka wa 18:

Basi katika kazi hiyo nilipokuwa nikienda Dameski,
mwenye mamlaka na maagizo ya wakuu wa makuhani; Ee Mfalme, ndipo wakati
wa adhuhuri njiani naliona nuru inatoka mbinguni ipitayo mwangaza wa jua,
ikinimulikia mimi, na wale waliofuatana nami pande zote. Tukaanguka nchi (chini)
sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya kiebrania, Sauli! Sauli!
mbona waniudhi? ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo (ujiti wenye ncha wa
kuchokolea). Nami nikasema,Wewe u nani, Bwana? Bwana akaniambia, Mimi ni Yesu,
ambaye wewe unaniudhi. Lakini inuka, usimame kwa miguu yako, maana
nimekutokea kwa sababu hii, nikuweke wewe uwe mtumishi na shahidi wa mambo haya
uliyoyaona, na wa mambo ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako;
nikikuokoa na watu wako, na watu wa Mataifa, ambao nakutuma kwao; uwafumbue
macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za
Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi
miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi.
Matendo 26.12-18
Sasa hapa tunaona khitilafu kubwa na zile ncha za hadithi ziliomo
katika sura ya 9 na sura ya 22 katika hicho hicho kitabu kimoja cha Matendo ya
Mitume. Hebu tuchungue:
- Kwa mujibu wa ncha hii si Paulo pekee aliyeona nuru - kama ilivyoelezwa pale mara ya kwanza - lakini wote waliokuwa naye waliona nuru, kama ilivyoelezwa mara ya pili.
- Hapa Paulo anasema: Tukaanguka nchi sote. Haya yanapinga ncha ya kwanza na ya pili zilizosema kuwa ni Paulo tu peke yake ndiye aliyeanguka chini.
- Katika masimulizi ya kwanza na ya pili ilisemwa wazi kuwa Paulo aliambiwa aingie mjini Demeski na huko ataambiwa habari za mambo yote yaliyoamriwa ayafanye. Hii mara ya tatu mambo yote ameamuriwa hapo hapo kabla ya kuingia mjini, kinyume na ilivyosimuliwa mara ya kwanza na ilivyosimuliwa mara ya pili. Tena hapo Paulo alimsikia Yesu anamuamrisha amri kinyume na alivyokuwa akiwafunza na kuwaamrisha wanafunzi wake siku zote katika uhai wake - anamuamrisha Paulo apeleke utume wa Yesu kwa mataifa mengine yasiyokuwa Mayahudi. Kadhaalika kinyume na mafunzo ya Yesu katika uhai wake anamuamrisha afunze kuhesabiwa haki kwa imani na kufutiwa dhambi.
Ni wazi kuwa Paulo kabla ya kutanasari kwake alikwisha jitayarisha
namna gani atavyougeuza Ukristo wa Yesu, waliokuwa wakiujua wote wanafunzi wake
kumi na mbili, uwe Ukristo wake yeye Paulo.
Na kwa nini Paulo aliongeza mengi aliposimulia mara hii ya tatu kuliko ilivyosimuliwa zile mara mbili za mwanzo? Ni kwa sababu hapa anasema na Mfalme Agripa. Lakini yafaa tusite na tujiulize: Nini thamani ya shahidi anayetoa ushahidi wake kwa polisi, akaubadilisha kidogo akifika kwa hakimu, na akatoa hadithi nyengine kabisa anapofika mahakama kuu kwa jaji? Hapana awezae kumueleza Paulo alivyo kama alivyojieleza mwenyewe katika barua yake aliyowapelekea Wakorintho. Amesema:

Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote,
nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi. Nalikuwa kama
Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya
sheria, nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya
sheria,) ili niwapate walio chini ya sheria. Kwa wale wasio na sheria
nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye
sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria. Kwa wanyonge nalikuwa
mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia
zote nipate kuwaokoa watu.
1 Wakorintho 9.19-22
Yaweza kuwa ni kweli kuwa mwenyewe Paulo akiamini kuwa hila hizo zote
azitendazo ni kwa ajili apate "kuwaokoa watu." Wengi miongoni
mwa wataalamu wa Biblia wanakubaliana na Dr.
Craveri na Dr. Schonfield kuwa makusudio ya Paulo ni kuwa apate yeye
binafsi wafuasi wengi zaidi ili apatekuwashinda wale wanafunzi wa Yesu
mwenyewe. Kwa hivyo ndio akawa hasikii haoni. Kwa lengo hilo yu tayari kufanya
lo lote, hata akakhiari kugeuza mafunzo ya Kristo ili apate wafuasi yeye
"kwa jina la Kristo." Kwa hakika wale wafuasi wake kutokana na
mataifa walibakia kuwa vile vile makafiri ila waligeuzwa jina tu, wakaitwa
Wakristo. Ndio hivyo alivyowaandikia Warumi:
Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na
katika moyo wako: yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo. Kwa
sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni
mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
Warumi 10.8-9
Ndio hivyo Ukristo umerahisishwa na Paulo ili isiwe taabu kwa makafiri
waweze kuitwa Wakristo bila ya kuufuata Ukristo wa Yesu. Katika mtindo huu
Paulo alipata upinzani kutokana na wengi, kama tunavyoona katika waraka wa Yakobo, nduguye Yesu,
unavyofunza imani ya matendo, si imani tupu. Natusome:
Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo
imani, lakini hana matendo? Je! ile imani yaweza kumwokoa? Ikiwa
ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, na mtu wa
kwenu akawaambia, enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini
asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini? Vivyo hivyo na imani, isipokuwa na
matendo, imekufa nafsini mwake. Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani,
nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha
imani yangu kwa njia ya matendo yangu. Wewe waamini ya kuwa Mungu ni
mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka. Lakini
wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?
Je! baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo
alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu? Waona kwamba imani ilitenda kazi
pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya
matendo yale. Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu,
ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki ya Mungu. Mwaona
kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani
peke yake. Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! hakuhesabiwa
kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia
nyingine? Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani
pasipo matendo imekufa.
Yakobo 2.14-26
Mafunzo haya yanapingana moja kwa moja na yale ya Paulo, na
yanakubaliana moja kwa moja na yale ya Yesu, mwenyewe. Si ajabu basi
kumsikia Paulo anakakamia kwa hasira isiyofichikana akisema:
Lakini nifanyalo nitalifanya, ili niwapinge hao
watafutao nafasi wasipate nafasi; ili kwamba katika neno hilo wajisifialo
waonekane kuwa kama sisi. Maana watu kama hao ni mitume wa uwongo,
watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa
Kristo. Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe
mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake hao wakajigeuza
wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.
2 Wakorintho 11.12-15
Ni dhaahiri kuwa Paulo anakusudia kwa matusi yake haya kuwatukana wale
wanafunzi wa Yesu, ambao Yesu mwenyewe aliwateua, ambao wakiongozwa katika
kutimiliza ujumbe wa Yesu na watu kama Yakobo, ambaye anaambiwa kuwa ni nduguye
Yesu. Je, sisi tutendeje tunapokabiliwa na maoni mbali mbali
yanayogongana miongoni mwa watu ambao wote wanadai kuwa ni wanafunzi wa Yesu,
ijapokuwa huyu mmoja Paulo, hata hakumwona Yesu, na huo ushahidi wa kuwa
kamwona katika njozi ni wake yeye tu, tena unagongana na kupingana wenyewe kwa
wenyewe? Tutendeje? Liliopo ni tuyaendee mafunzo yake mwenyewe Yesu,
ambayo ijapokuwa yametatanishwa na maongezo na mapunguzo, lakini hayaachi
kuwepo ya kutosha kwa jumla kutufahamisha nini khasa mafunzo yake. Ikiwa
kweli tunatafuta hakika ya mambo na ukweli wake basi tutayachukua yale yalio
wazi, dhaahiri, katika maneno yake mwenyewe Yesu, na tusiyakubali yale ambayo
ni maneno ya wasimulizi. Kadhaalika yasitushughulishe yale ya mafumbo
yanayotatanisha tukajaribu kuleta tafsiri na maelezo tuyapendayo nafsi
zetu. Ikiwa ni kufasiri basi tufasiri fumbo kwa kauli ya Yesu ilio wazi.
Wapotoshaji hufanya kinyume cha hayo.
Mafundisho yaliyotulia kabisa ya Yesu ni yale aliyohubiri juu ya Mlima wa Zaituni. Na maoni yake yaliyo wazi na kauli ya kukata juu ya sharia na matendo, ni yaliyomo katika sura 5 ya Mathayo. Akizungumzia juu ya wale wanaodai kuwa wao ni wafuasi wake, na kuwa ati wanafunza mafunzo yake, na huku kumbe wanayapotoa yale aliyoyafunza, Yesu anaambiwa kasema:

Si kila mtu aniambaye, Bwana, Bwana, atakayeingia
katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu
aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana,
hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako
kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe
ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. Basi kila asikiaye hayo maneno
yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake
juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga
nyumba ile isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya
mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na
mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha,
mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo
anguko lake likawa kubwa.
Mathayo 7.21-27
Hayo ni maneno aliyokhitimishia Yesu mawaidha yake juu ya Mlima wa
Zaituni. Ni maneno yaliyokaa sawa, yawazi, hayana ubabaishi. Ni
nani hao "watendao maovu", hao wapumbavu, wasiofuata mafunzo ya Yesu
wakayatenda, mafunzo ambayo msingi wake ni kutimiliza sharia na manabii, na
kutenda mapenzi ya Mungu? Ni nani hao wanaodai kufanya miujiza na
kuponyesha watu kwa jina la Yesu, na kudai kuwa ni mitume wa Kristo, na huku
wanapinga mafunzo yake, na kuwaambia watu kuwa wataokoka kwa imani tu kwamba
Yesu kafa msalabini kwa ajili yao, bila ya haja ya vitendo? Ni nani hao
wanaolitumia jina la Yesu naye mwenyewe atawakataa? Kama tuna akili basi
yafaa tuitumie. Tusiwe kama mtu mpumbavu ajengaye nyumba yake juu ya
fungu la mchanga. Tutaanguka, na anguko letu litakuwa kubwa.
Mafunzo ya Yesu Kristo si haba, lakini kwa ufupi wa maisha yake (aliwahi kuhubiri kiasi miaka miwili mitatu tu) na kutokuwa tayari ulimwengu kuchukua kweli yote, hakuweza kutimiza ujumbe wote wa Mwenyezi Mungu. Ni hikima yake Mwenyezi Mungu kuwa kila nabii aliyemleta alikuwa anaongeza juu ya yale yaliyotangulia. Ni kweli Yesu alisema kama ilivyo katika Mathayo 5.17-20 ambayo tumekwisha yataja kuwa yeye alikuja kutimiza Taurati na mafunzo ya Manabii, hakuja kutengua lo lote katika hayo. Ulipokaribia wakati wake wa kuondoka aliungama kuwa mengi aliyo nayo hana nafasi ya kuyasema, lakini atakuja mwenginewe ambaye atauwongoza ulimwengu kwenye kweli yote, na ataufundisha ulimwengu mafunzo kaamili juu ya dhambi na haki.
Injili ya Yohana inanukulu maneno ya Yesu:

Lakini sasa mimi naenda zangu kwake yeye
aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizaye, Unakwenda wapi!? Ila
kwa sababu nimewaambia hayo huzuni imejaa mioyoni mwenu. Lakini mimi
nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke; kwa maana mimi
nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu,
nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa
habari ya dhambi, na haki, na hukumu. Kwa habari ya dhambi, kwa sababu
hawaniamini mimi; kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba,
wala hamnioni tena; kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa
ulimwengu huu amekwisha hukumiwa. Hata bado nikali ninayo mengi ya
kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahamili hivi sasa. Lakini yeye atapokuja huyo
Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena
kwa shauri lake mwenyewe lakini yote atayoyasikia atayanena, na mambo yajayo
atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi; kwa kuwa atatwaa katika
yaliyo yangu na kuwapasha habari.
Yohana 16.5-14
Kwa mujibu wa maneno hayo kama ilivyo katika Injili ya Yohana, Yesu
anawaambia wanafunzi wake kuwa yeye yu karibu kuondoka duniani, na ya kwamba
hajatimiza ujumbe wake, lakini atakuja mwenginewe ambaye ameitwa majina mbali
mbali kwa mujibu wa tafsiri mbali mbali za Biblia. Hapa anaitwa Msaidizi
katika tafsiri hii ya Kiswahili inayoitwa Union
Version. Kwa mujibu wa tafsiri ya zamani ya Kiingereza, King James's Authorised Version, anaitwa Comforter, yaani Mliwazi; na
kwa mujibu wa tafisiri nyengine ya Kiingereza ya kisasa Revised Standard Version, anaitwa
Counsellor, yaani Mshauri, na tafsiri nyengine mpya mpya za
Kiingereza anaitwa Helper, ambayo maana yake
pia ni Msaidizi. Tafsiri ya Kiarabu ya Darul
Kitabul Muqaddas ya Cairo anaitwa Al
Mu'azzi yaani Mliwazi. Vyo vyote vile iwavyo huyo Msaidizi, au
Mliwazi, au Mshauri, ameelezwa na Yesu kwamba:
- Atakuja baada yake Yesu, yaani wakati huo hayupo;
- Atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki na hukumu;
- Atauongoza ulimwengu autie kwenye kweli yote;
- Hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini atakayoyasikia atayanena;
- Atatoa khabari ya mambo yajayo;
- Atabakia nasi milele;
- Atamtukuza Yesu Kristo.
Hebu natuichungue bishara hii ya Yesu bila ya chuki, bila ya
mapendeleo, na bila kutiwa pingu na mawazo tuliyofungwa nayo tangu
utotoni. Sasa tu watu wazima na tuna akili zetu, natuzitumie. Wakristo
wengi wanachukulia kuwa huyo Msaidizi ni Roho Mtakatifu, nafsi ya pili ya
Mungu. Hivyo ndivyo walivyofundishwa Kanisani na mapadri. Imani hii
yazidi kutiliwa nguvu na hiyo kauli "huyo roho Mtakatifu" iliotiwa
kati baada ya neno "Msaidizi" liliomo katika mstari wa 26 sura ya 14 ya
hii Injili ya Yohana. Hapana lawama basi kuwa baadhi yetu tukawa tunaamini kuwa
Yesu ametwambia katika Yohana 14 na 16 kuwa atakuja Roho Mtakatifu ndiye
atayetuongoza na kutufundisha yote yaliyobaki sisi kufunzwa, na ambayo yeye
Yesu hakuwa na wakati kufundisha au watu wakati ule walikuwa bado hawajawa
tayari kuyapokea. Kwa kuwa Roho Mtakatifu anaongoza Kanisa la Yesu (yaani
ndio Mapadri, tangu Baba Mtakatifu mpaka Maaskofu na Mapadri wote, na Wazee wa
Kanisa, na Wachungaji) ndio Wakristo hawana wasiwasi wala hawajiulizi kwa
nini leo wanafundishwa mambo ambayo Yesu hakuyafundisha, na wanapewa amri, au
kukatazwa jambo, ambalo Yesu hakuliamrisha au hakulikataza. Roho Mtakatifu ni
Nafsi ya Mungu, ni sawa sawa na Yesu, basi ana madaraka kuendelea kufunza,
kuamrisha na kukataza, kama Yesu, Mungu Mwana, na Mwenyezi Mungu, Mungu
Baba. Yesu alionekana na watu walimwona. Alisema na maneno yake
yameandikwa. Lakini Roho Mtakatifu ananon'gona na Mapadri tu na Wakristo
wanafuata wanayoambiwa na Kanisa, yaani Mapadri. Si ajabu kuona wanaojiita Wakristo
wanafuata Kanisa zaidi kuliko kumfuata Yesu Kristo mwenyewe kwa sababu
wamejazwa katika akili zao kuwa nafsi ya pili ya Mungu ipo Kanisani ikiendeleza
kuugeuza Ukristo wa Yesu kama ipendavyo hiyo nafsi. Lakini natuyazingatie haya:
Kwa mujibu wa imani ya Kanisa, Roho Mtakatifu ni Mungu, ambaye ni sawa na Mungu Baba, na Mungu Mwana. Tumeona katika maneno ya Yesu kuwa Msaidizi atakuja baada yake Yesu, yaani wakati huo hakuwako. Je, tuseme kuwa wakati wa Yesu hakuwako Mungu Roho Mtakatifu? Mbali ya kuwa Roho ameelezwa mara nyingi sana katika Agano la Kale, na kuwa ndio akiwaongoza manabii wote, bali Wakristo wanaamini kuwa waandishi wote wa vitabu vya Biblia, kabla na baada ya Yesu, waliongozwa na Roho Mtakatifu. Tunasoma humu humu katika Injili ya Yohana sura ya kwanza mstari wa 32:

Tena
Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka
mbinguni; naye akakaa juu yake (Yesu).
Yohana 1.32
Tena tunasoma katika Injili ya Marko:
Mara Roho akamtoa (Yesu) aende nyikani. Marko
1.12
Na tunaona katika Luka:
Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa
divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa
mamaye. Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao.
Luka 1.15-16
Roho Mtakatifu daima yu pamoja
na Yesu, hangojei kuondoka kwake ndio aje. Alikuwa na Yohana Mbatizaji (Nabii
Yahya) tangu tumboni mwa mamaake. Luka hapo anatupa ushahidi kuwa
Yohana hakupata kunywa divai wala kileo "kwa sababu atakuwa mkuu mbele ya
Mungu" . Ni nani, basi aliyewahalalishia Wakristo kunywa ulevi, hata
ikawa ibada yao haitimii ila wanywe mvinyo? Labda ni Paulo akiongozwa na
Roho Mtakatifu. Ni kweli wafuasi wa kweli wa Yesu sio wale wapigao kelele,
Bwana, Bwana, sisi twaamini uokozi wa damu yako. Wafuasi wake wa kweli ni wale
wanaotenda aliyofundisha, na wanaokwenda mwendo wake. Hao hata hawana haja ya
kujiita Wakristo.
Si kama Roho Mtakatifu alikuwa na Yesu tangu tumboni mwa mamaake tu kama Yohana, bali tunaambiwa na Injili ya Mathayo kuwa hiyo mimba yenyewe kaichukua mama yake, Mariamu, "kwa uweza wa Roho Mtakatifu." (Mathayo 1.18).
Ni wazi kabisa kuwa Roho Mtakatifu hakungojea Yesu aondoke ndio aje, bali daima milele yupo, kwa ushahidi wa Biblia yenyewe. Kwa ushahidi huu tu tunayakinika kuwa huyo Msaidizi ajaye, siye Roho Mtakatifu, nafsi ya pili ya Mungu.
Tena tunaambiwa kuwa Roho Mtakatifu ndiye anayeongoza Kanisa mpaka hii leo. Lifanywalo na lisemwalo na Kanisa basi ni kwa uwongozi na ufunuo wa Roho Mtakatifu, huyo aliyebashiriwa na Yesu kama ilivyosimuliwa katika Injili ya Yohana. Lakini ilivyokuwa Ukristo ulivyogawika katika makanisa, au madhehebu, yasiokuwa na hisabu, na kila kanisa linafunza mambo ambayo tangu msingi wake yanakhitalifiana na mengineyo, jee ni madhehebu gani, au kanisa gani, linaloongozwa na Roho Mtakatifu.
Kama wote hao wanaongozwa na Roho huyo huyo basi mbona wanagongana katika mambo ya msingi? Bali hata kanisa moja, mathalan, Kanisa Katoliki la Roma, ndilo kubwa lao na lenye nidhamu kuliko yote, mbona mara nyingi hugeuza geuza maoni yake?

Zamani tulipokuwa wadogo ilikuwa mwiko kwa Wakatoliki kula nyama siku
ya Ijumaa, kwa kuwa ndio siku aliyotundikwa Bwana Yesu. Sasa ni halali kwao.
Zamani ilikuwa mwenye kuwa na wake zaidi ya mmoja alitengwa, na wala hapati
ibada fulani za sakramenti, kama Kushiriki katika Chakula cha Bwana. Leo
wanakubaliwa, na inakubaliwa kuwa kuoa mke mmoja si sharia ya Kikristo bali ni
mila za Kizungu zilizoingizwa katika dini. Aliyewazindua Wazee wa Kanisa ni
Roho Mtakatifu? Ikiwa ni yeye kwa nini huyo Roho Mtakatifu alinyamaza
kimya miaka yote hiyo? Wangapi waliotengwa na Kanisa, wakalaaniwa, na
wakachomwa moto hadharani, na baadae watu hao hao baada ya miaka kupita wakaja
wakatakaswa na kubarikiwa na kutangazwa na Kanisa lile lile kuwa niWatakatifu?
Na wakati huo huo tuone ni Roho Mtakatifu, Mungu, asiyekosea, ndiye amelijaa
Kanisa na analiongoza! Bila ya shaka huyu siye aliyebashiriwa na Yesu.
Kanisa la Roma linasema ni haramu kwa padri kuoa. Hivi sasa wapo mapadri si
chini ya 80,000 duniani wa Kanisa la Roma ambao wana wake, miongoni mwao 18,000
wako Amerika (U.S.A.). Si ajabu kutokea siku yo yote kuwa Baba Mtakatifu, huku
akiongozwa na Roho Mtakatifu, akiona mambo ni ya mno, akatoa amri kuwa sasa ni
halali kwa mapadri kuoa bila ya kificho, na bila kuleta nuksani yo yote.
Yesu ametwambia kuwa huyo ajaye hatanena kwa shauri lake mwenyewe. Je, Roho Mtakatifu, ambaye ni Mungu, hunena kwa shauri ya nani? Mungu hunena anayoyasikia au hunena yake mwenyewe? Ikiwa hunena anayoyasikia, basi anayasikia kwa nani? Kwa Mungu Baba, au kwa Mungu Mwana, na hali tunaambiwa katika Utatu, nafsi zote tatu ni sawa. Ikiwa yeye ni Roho Mtakatifu, ambaye ni Mungu, pana lipi la ajabu hata ihitajie Yesu kusema kuwa atatoa habari ya mambo yajayo? Hapana ajabu Mungu kuagua yajayo, na hali ni Yeye aliyeyaumba.
Huyo ajaye, Yesu anasema, atamtukuza Yesu. Kwani Mungu Mwana ana haja gani ya kutukuzwa na Mungu Roho?
Hayo yote tukiyazingatia kwa nia safi tutaona kuwa hayamuelekei Roho Mtakatifu, ambaye ni Mungu kama lisemavyo Kanisa, hata chembe. Je, kama bishara hii haimuelekei Roho Mtakatifu, inamuelekea nani? Ni mtu gani huyo ambaye alikuja ulimwenguni baada ya kuondoka Yesu, akauhakikisha ulimwengu kwa khabari ya dhambi na hukumu, akauongoza ulimwengu na kuutia kwenye kweli yote, akawa haneni kwa shauri lake wala mapenzi yake bali husema kwa aambiwayo na Mwenyezi Mungu, akatoa khabari ya dhambi na mambo yajayo, akatwachia mafunzo katika Kitabu kisichobadilika milele na mafunzo yake yakakaa nasi milele mpaka mwisho wa dunia, akamtukuza Yesu Kristo? Katika historia yote hakutokea mtu mwenye kukusanya sifa zote hizo ila NABII MUHAMMAD tu.
Mtume Muhammad s.a.w. ndiye aliyekuja baada ya Nabii Isa a.s. Yeye peke yake katika Manabii na Mitume wote ndiye aliyesema maneno ya kutimiza ujumbe wote wa Mwenyezi Mungu, ndiye aliyeleta kweli yote. Kila Nabii aliyetangulia alibashiri kuja mwinginewe baadae. Musa alisema hayo, na Yesu kasema hayo, na wenginewe wote wamesema. Ila Nabii Muhammad ndiye aliyesema: "Hapana Nabii baada yangu." Na Mwenyezi Mungu alimwambia karibu ya kufa kwake:

Leo waliokufuru wamekata tamaa katika Dini yenu,
basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamilishieni Dini yenu,
na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini.
(Qur'ani) Al Maida
5.3
Mwenye kukamilishiwa Dini na kutimiliziwa Neema, amekamilishiwa na
kutimiliziwa kila kitu: ndiyo kweli yote, na hukumu na khabari ya dhambi.
Ni Muhammad ndiye ambaye alikuwa akijuulikana hata na maadui wake kuwa ni msema
kweli, wa kuaminiwa, Assaadiq, Al Amin, "Mkweli Muaminifu" na kweli ndiye Roho
wa kweli.
Huyo ajaye, Yesu anatwambia, hatanena kwa shauri lake. Ni Mtume Muhammad, peke yake, ndiye ambaye historia inatwambia kuwa mafunzo yake ni maneno ya Mwenyezi Mungu. Qur'ani Tukufu yote ni maneno ya Mungu, moja kwa moja. Qur'ani haikutungwa na Muhammad wala na ye yote katika wanaadamu. Sio kama vitabu vya Biblia, ambavyo vinajuulikana vimeandikwa na watu fulani kama vile Injili ya Mathayo, ya Marko n.k. na Torati ya Musa. Hii ni Qur'ani ya Mwenyezi Mungu, si ya Muhammad. Kama isemavyo hiyo Qur'ani:

Arrahman (Mwingi wa Rehema) amefundisha Qur'ani.
(Qur'ani) Arrahman 55.1-2
Na
ilivyobainishwa katika Sura An Najm:
Wala (Muhammad) hasemi kwa matamanio. Hayakuwa haya
ila ni ufunuo uliofunuliwa; amemfundisha Mwenye nguvu kweli.
(Qur'ani)
Annajm 53.3-5
Na ilivyosemwa katika Sura An
Nisaa:
Hawaizangatii
Qur'ani? Na lau kama imetoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka
wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi.
(Qur'ani)
An Nisaa 4.82
Mkristo wa Kiingereza, Dr. John B. Taylor,
Mwalimu wa Masomo ya Kiislamu katika Chuo cha Birmingham,
ameandika katika kitabu chake: Thinking About Islam (Kuufikiria Uislamu):
"Tumethibitisha
ya kuwa Waislamu hawasemi kuwa Muhammad ndiye aliyeandika Qur'ani, lakini kuwa
yeye ameipokea na akaisoma. Kama alivyokuwa Muhammad mwenyewe
akishughulika mno kuyaweka safi maandiko (matini) ya Qur'ani, basi hali
kadhaalika wale Waislamu waliokuja baada yake walifanya juhudi kuhifadhi
bila ya kukosea ko kote vipande mbali mbali vya Qur'ani. Miaka miwili tu
baada ya kufa Muhammad, kwa kuwa walikufa vitani baadhi ya wale waliokuwa
wameihifadhi kwa moyo, sehemu mbali mbali za Qur'ani zilikusanywa...
"Baada
ya miaka michache, katika enzi ya Uthman, Khalifa wa tatu kuwatawala Waislamu
baada ya Muhammad, ilipitiwa mara ya mwisho kusahihishwa matini ya
Qur'ani. Twaweza kutambua vipi walivyokuwa na hadhari kubwa wale Waislamu
wa mwanzo kwa vile hata kukhitalifiana matamshi baina ya sehemu moja ya nchi za
Kiislamu na nyengine, hakukuruhusiwa. Kwa hivyo yale maandishi ya rasmi
yakathibitishwa kufuata lafdhi ya Makka, na zile ziliobaki zikateketezwa kwa
amri ya Khalifa. Kwa hivyo tunaweza kuwa na yakini kuwa hii Qur'ani tulio
nayo hii leo, kama iwezekanavyo kibinaadamu, ndio ile ile iliyothibitishwa
miaka michache tu baada ya kufa Mtume."
Hayo ni maneno ya Mkristo ambaye kazi yake ni kuutafutia ila na nuksani Uislamu. Qur'ani ni neno la Mwenyezi Mungu lisio na upungufu wo wote kwa sababu ni maneno yake mwenyewe. Hayo ndiyo makusudio ya Yesu aliposema kuwa huyo Msaidizi ajaye, "hatanena kwa shauri lake mwenyewe."
Yesu kadhaalika ametwambia kuwa Msaidizi atakayekuja atatoa khabari ya mambo yajayo. Kila alilosema Mtume Muhammad s.a.w. kuwa litakuja basi limetokea vile vile alivyosema. Katika alilosema ni kuwa Warumi baada ya kushindwa na Waajemi wao watakuja shinda mnamo miaka michache na hapo Waislamu watafurahi. Na kweli walishindwa Waajemi mwaka 624 B.K. na ndio mwaka Waislamu walipowashinda makafiri wa Kikureshi katika vita vya Badru.
Mtume alipokubali mkataba wa suluhu pale alipozuiliwa kuingia Makka alisema kuwa Waislamu watakuja kuikomboa Makka karibuni, na hakika hivyo ndivyo ilivyokuwa baada ya miaka miwili, na ikawa ndio ushindi ulioenea Arabuni kote.
Mtume Muhammad alipokuwa akichimba handaki, pamoja na Masahaba zake, kuilinda Madina na maadui, kulimetuka cheche tatu alipokuwa akipiga mtaimbo kulisukua jiwe. Cheche moja ilielekea kusini, Mtume akasema Yaman itasilimu. Cheche ya pili ikaelekea mashariki, na Mtume akasema Iran itasilimu. Cheche ya tatu ilipometukia kaskazini Mtume s.a.w. akasema Sham iliyokuwa chini ya utawala wa Kikristo wa Kirumi itasilimu. Na zote zikaja kusalimu amri na kusilimu hivyo hivyo kama alivyobashiri, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, katika zama ambazo Warumi walikuwa ndio kama Marekani walivyo sasa, na Waajemi ndio kama Warusi walivyo sasa. Hizo ndizo dola kubwa kabisa, na Muhammad ni bedui mnyonge ambaye ndiye kwanza kachipuka huko jangwani akiwahubiria makafiri wa miji miwili midogo kabisa Makka na Madina. Na mengi, kabisa, aliyokuwa akiyasema Mtume Muhammad s.a.w. na yote yalikuwa hayaanguki chini. Nimeyataja hayo ambayo yamo katika vitabu vya historia vilivyoandikwa hata na wasiokuwa Waislamu.
Yesu tena amesema huyo Msaidizi "atanitukuza mimi." Na kweli Yesu Kristo au Isa Masihi (wamuitavyo Waislamu) alitukanwa na maadui zake, Mayahudi, kwa kumwambia kuwa ati ni mwana haramu, mzushi, mlaanifu. Wakidai kuwa uthibitisho wa laana hiyo ni kuwa waliweza kumwua kwa kumtundika msalabani. Taurati ilisema kuwa ye yote anayekufa kwa kutundikwa kwenye mti basi amelaanika, na hayo ndiyo yalikuwa makusudio yao. Hali kadhaalika waliokuwa wakijiona kuwa ni wafuasi wake Yesu watiifu walimvunjia daraja yake kwa kukubali madai ya Mayahudi kwa kuwa alikufa msalabani, na pia kwa kumfanya yeye ni sawa na ile miungu ya bandia ya uwongo sawa na ya akina Mithra, na Apollo, na Osiris ya kipagani, na kwa kumtoa kwenye cheo chake kitukufu ambacho yeye mwenyewe alikuwa akitafakhari nacho kama isemavyo Biblia. Daima Yesu akitafakhari na kujiita yeye ni mwanaadamu, mtumishi wa Mwenyezi Mungu, ambaye hawezi kusema kitu wala kutenda kitu ila kama anavyoamrishwa na Mungu. Yesu akitafakhari kuwa ni Nabii wa Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, sio kuwa mungu kama miungu iliyojaa katika pande zile kwa zama zile. Hata wafalme madhaalimu wa Kirumi walikuwa wakiitwa miungu. Wao hao wajiitao Wakristo waliacha kufuata mafundisho yake Yesu na kuyatenda, na badala yake wakafuata mafundisho ya wale wale washirikina ambao Yesu kaja kuwapinga. Ndio maana akasema: "Wengi watanambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitwaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu."
Ni kwa kupitia Mtume Muhammad, huyo Msaidizi aliyetwambia Yesu kuwa atakuja kumtukuza, ndio tunasoma maneno ya Qur'ani Tukufu:
Enyi watu
wa Kitabu (yaani Biblia)! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msiseme
juu ya Mwenyezi Mungu ila yaliyo kweli. Hakika Masihi, Isa bin Maryam, ni
Mtume wa Mwenyezi Mungu na neno lake alilompelekea Maryam, na ni roho iliyotoka
kwake. Basi mwaminini Mwenyezi Mungu na
Mitume yake; wala msiseme, "Watatu". Wacheni! Itakuwa
kheri kwenu. Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu.
Ametakasika Yeye kuwa na mwana. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo
duniani; na Mwenyezi Mungu ni mtegemewa wa kutosha. Masihi hataona
uvunjifu kuwa mtumwa wa Mwenyezi Mungu, wala Malaika waliokurubishwa. Na
watakaouona uvunjifu utumwa wa Mungu na kufanya kiburi, basi atawakusanya wote
kwake.
(Qur'ani)
An Nisaa 4.171-172
Katika Sura Al Imran tunasoma vipi alivyotukuzwa
Yesu:
Waliposema
Malaika: Ewe Maryam! Mwenyezi Mungu anakubashiria kwa neno litokalo
kwake, jina lake ni Masihi Isa, mwana wa Maryam, mwenye hishima katika dunia na
Akhera, na miongoni mwa waliokaribishwa (kwa Mungu). Naye atazungumza na watu
katika utoto wake na katika utuuzima wake, na atakuwa katika watu wema.
(Maryam) akasema: Mola wangu! Vipi nitampata mtoto na hali hajanigusa
mwanaadamu ye yote? Akasema: Ndivyo vivyo hivyo, Mwenyezi Mungu huumba
apendacho; anapohukumu jambo, huliambia: Kuwa, basi huwa. Na atamfunza
Kitabu na Hikima na Taurati na Injili. Na ni Mtume kwa wana wa
Israili.
(Qur'ani) Al Imran
3.45-49
Na kabla ya aya hizi inasimuliwa vipi alivyoteuliwa mama yake Yesu na
kutukuzwa:
Na Malaika
waliposema: Ewe Maryam, kwa hakika Mwenyezi Mungu amekuteuwa na
kakutukuza kuliko wanawake wa ulimwengu.
(Qur'ani) Al Imran 3.42
ANGAZA
ANGAZA
ANGAZA
0 comments:
Post a Comment