BWAKWATA YAMUUNGA MKONO JOHN MAGUFULI


Tanga. Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), limewataka watendaji wanaopewa dhamana na Taifa ya kusimamia mikataba ya miradi mikubwa, kuweka mbele uzalendo badala ya kuingia mikataba yenye kuwezesha rasilimali za nchi kuporwa. 

Baraza hilo limeahidi kumuunga mkono Rais John Magufuli katika vita hii ya kupambana na uporaji wa rasilimali za umma kwa kuwa anafanya kazi inayompendeza Mungu kwani hataki mali za wanyonge zichukuliwe na wenye nguvu. 

Sheikh wa Bakwata, Mkoa wa Tanga, Ali Jumaa Luwuchu ameyasema hayo leo Alhamisi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na  ripoti ya  pili ya kamati ya kuchunguza mchanga wa madini kwa upande wa kisheria na kiuchumi. 

“Viongozi wa dini tunamuombea dua njema ili Mungu  ampe nguvu katika vita ya kupambana na maovu siyo katika sekta ya madini pekee, bali hata biashara  ya dawa za kulevya, kuhimiza kila mtu afanye kazi na suala zima la rushwa,” amesema Sheikh Luwuchu. 

Luwuchu ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya baraza la amani  na kadhi wa Mkoa wa Tanga, amesema chanzo cha uporwaji wa rasilimali za Taifa ni kukosa uzalendo na uadilifu kwa wanaopewa dhamana ya kusimamia michakato ya mikataba kati ya nchi na wawekezaji. 

Amesema kazi iliyofanywa na Rais Magufuli katika sakata la makinikia limewafumbua macho wananchi kwamba kumbe kama rasilimali zilizopo zikitumika vizuri, Tanzania inaweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo kuliko ilivyo hivi sasa. 
Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment