TRUMP UNATAKA NINI LAKINI!!!!!!!!!?

Raia kutoka mataifa sita ya nchi za Kiislamu na wakimbizi wote sasa wanakabiliwa na masharti magumu ya kuingia nchini Marekani kufuatia marufuku ya rais Trump ambayo imezua utata. 

Hii inamaanisha kwamba watu wasio na uhusiano wa karibu na wale wanaoishi Marekani ama uhusiano wa kibiashara nchini Marekani huenda wakanyimwa Visa na kuzuiliwa kuingia. 

Bibi, shangazi, mjomba ,binamu na mpwa hawakubaliki kuwa watu wenye uhusiano wa karibu na mtu anayetaka kuingia taifa hilo. 

Sheria hiyo itawaathiri raia wanaoishi Iran, Syria, Somalia, Sudan na Yemen pamoja na wakimbizi wote. 

Muda mfupi kabla ya marufuku hiyo, ilibainika kwamba jimbo la Hawaii lilikuwa limemuuliza jaji mmoja wa kijimbo kufafanua sheria hiyo. 

Jimbo hilo awali limekuwa likiishutumu serikali ya Marekani kwa kukiuka sheria ya mahakama ya juu kupitia kuwatenga watu. 

Kuzuia raia wa baadhi ya nchi za kiislam ilikua moja ya ajenda za Trump wakati wa kampeni za urais 
Mapema wiki hii, mahakama ya juu ilikubali marufuku hiyo kutimizwa kwa muda hatua iliositisha sheria iliowasilishwa mahakamani kuzuia sera hiyo muhimu ya Trump. 

Mahakama iliamuru kwamba watu wanaotafuta Visa kuingia Marekani kutoka mataifa hayo sita pamoja na wakimbizi wote, watalazimika kuthibitisha kuwa na uhusiano wa karibu na raia wa taifa hilo . 

Mahakama ya juu inatarajiwa kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu marufuku hiyo mnamo mwezi Oktoba. 

Kulingana na sheria hiyo mpya, katika kipindi cha siku 90 zijazo raia kutoka mataifa hayo sita wasio na uhusiano wa karibu na raia wa Marekani hawataruhusiwa kuingia nchini humo. 

Wale watakaoruhusiwa ni wale walio na wazazi wao, mke au mume, mtoto wa kiume ama wa kike na mwana wa kambo. 

Pia wale wasio na uhusiano wa kibiashara au ule wa masomo na Marekani hawataruhusiwa kuingia. 
Hatahivyo maelezo hayo yanasema kuwa uhusiano huo ni sharti uwe kwa njia rasmi, ulionakiliwa na sio kwa lengo la kukwepa agizo hilo. 

Wale walio na Visa hawataathiriwa.Wale wenye uraia wa mataifa mawili wanaotumia pasipoti zao pia wataruhusiwa.
Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment