IKIWA UKUSWALI WALA UKUSADIKI YA MITUME NA MANABII.


Mara nyingi Mwanadamu amekuwa kiumbe cha kupita dunia na hii haina shaka kwamba pale afikiwapo na umauti atarejea kwa yule aliyemuumba naye si Mwingine bali Mwenyezi Mungu(Subhaanahu Wa Ta’ala)  Japokuwa mwanadamu yumo katika maangaiko hapa duniani ya kuchuma mali, watoto,wanawake'' Lakini tazama saa inakuja ambapo atafikwa na Umauti..........Wala hakitomfaa kitu kati ya yale aliyokuwa anayapenda hapa duniani. Wala hatomfaa Mzazi, Watoto,Jamaa, Ndugu, Mke hata mali hazitomfaa chochote wakati wa kutolewa Roho yake. Na ikiwa umefikwa na Mauti hsli ya kuwa umo ndani ya Uovu ni uzuni hapa duniani na Akhera maana  kuhusu mtu muovu yeye atakaa katika kaburi lake kwa khofu na fadhaa huku akisubiri hukumu ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu Wa Ta’ala) Huku  akiulizwa: Ulikuwa katika nini wakati ukiwa hai? Atajibu sijui. Kisha ataulizwa tena: Je wakati huko hai ukufikiwa na waonyaji? Atajibu hakika nilijiwa na waonyaji ila nikayakadhibisha waliyokuwa wakinieleza. Hapo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu macho yake yataduwaa huku akiona waziwazi yale aliyokuwa akiyakanusha nayo ni Pepo na Jehanamu kisha atauona uwazi wa kumuwezesha kuiona pepo ataangalia na kuona uzuri wake na vilivyomo ndani yake. Ataambiwa: Angalia kile ambacho Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Amekukosesha (Kutokana na Imani yako mbovu ya kuwakanusha mitume na kuyakataa aliyokuja nayo Nabii wa Mwenyezi Mungu huku ukimshirikisha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu Wa Ta’ala). Kisha utawekwa uwazi wa kumuwezesha kuona Jehanamu kisha aambiwe  hii ndio sehemu yako ambayo uliendesha maisha yako kwa kuwa ukusadiki wala ukuswali, ukutoa zaka, nawe ukayakadhibisha aliyokuja nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu  na mashaka nayo yalikujaa  , Na umekufa ukiwa na mashaka  na utafufuliwa ukiwa katika hali hiyo hiyo,     

     in shaa Allaah”. [MWENYEZI MUNGU ATUOKOE].          
Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment