((Mja katika waja wa Allaah alisema: Ewe Mola wangu! Zako wewe tu sifa zote njema Unayestahiki kushukuriwakama inavyopasa Utukufu Wako na nguvu Zako kubwa kabisa. Malaika wawili walibabaika hawakujua vipi waandike maneno hayo (jinsi alivyomtukuza utukufu wa Mola wake) Wakaenda kwa Allaah wakasema: Ewe Mola wetu! Hakika mja wako kasema aliyoyasema na wala hatujui vipi tuyaandike. Akasema Allaah: Kwani kasema nini mja wangu? (Na Allaah Anajua aliyoyasema mja Wake bila ya malaika kumwelezea) Wakasema amesema: Ewe Mola wangu! Zako Wewe tu sifa zote njema Unayestahiki kushukuriwa kama inavyopasa Utukufu Wako na nguvu Zako kubwa kabisa. Allaah akasema: Yaandikeni kama alivyosema mja Wangu mpaka atakaponikuta (siku ya malipo) basi nitampa jazaa yake kwa hayo (aliyoyasema) )) [Ibn Maajah 2:1249]