VUKA NA HAYA ILI USHINDE

Siku ya leo ningependa kuchukua fursa hii niweze kukushirikisha mambo mbalimbali ambayo yataweza kukuondoa kutoka sehemu moja hadi nyingine ya kimafanikio.Yapo mambo mbalimbali ambayo watu waliofanikiwa waliyafanya hivyo basi na sisi leo hii tukiyafanya tutafanikiwa kimaisha. Mafanikio ya kimaisha huja kwa kuiweka akili yako kuweza kupambana na changamoto za kimaisha na hatimaye kuona mwanga wa mafanikio.

Yafuatayo ni mambo ya msingi ya kuzingatia ili nasi tuweze kufanikiwa;

1.Tazama fursa zilizopo
Mpenzi msomaji wangu wa makala hii jitahidi kuzitazama fursa zilizopo katika eneo lako unaloishi au nje ya eneo lako unaloishi.Fursa zilizopo ni chanzo kikubwa cha utajiri wa kimafanikio.Nasema hivi ni kiwa na maana ya kwamba fursa mara nyingine hutoka na changamoto zilizopo eneo fulani, fursa hizi huenda zikawa ni mahitaji ya watu.Nasema hivi ni kiwa na maana ya kwamba kwa mfano mtaani kwako kuna tatizo la eneo la kutupa taka taka unaweza ukachukua kama fursa hiyo na kuanza kupita kwa makazi ya watu na kuchukua taka hizo na kwenda kuzihifadhi eneo husika na hatimaye wakazi hao kukulipa kiasi cha fedha.Na vilevile kila changamoto zilizopo eneo furani ni fursa ya kuweza kupata kipato na hatimaye kuona fursa ya mafanikio.

2.Jiamini wewe mwenyewe
Mafanikio huja kutokana na hofu kufa.Wapo watu mbalimbali ambao hutafuta ushauri kwa watu waliofanikiwa hilo ni jambo nzuri.Weka jitihada zako wewe mwenyewe kuwa unaweza kufanikiwa. Kuwa na mawazo chanya yenye kuleta maono ya kufanikiwa hapo baadae.Hakuna dhambi kubwa kama kukata tamaa jiamini kuwa unaweza ama hakika utafanikiwa’’maisha siyo magumu ila sisi ndio wagumu na daima siku zote kitu rahisi ndicho sahihi’

3.Acha kusikiliza maneno ya watu wanao kukatisha tamaa
Wapo baadhi yawatu ambao wapo kwa ajili ya kuwakatisha watu wengine tama.Hivyo basi kama wewe ni kweli unahitataji mafanikio najua yapo mengi yatasemwa juu yako kwa ajili ya kukuvunja moyo.Wewe wasikilize lakini achana na mawazo hasi ambayo hayana tija kimafanikio.Kuwa ni mtu wa kusikiliza mawazo chanya yenye kuleta njia sahihi ya kuona maono ya kimafaniko.Kuwa makini katika kuchagua marafiki sahihi wenye mawazo yakinifu yenye kuleta mtazamo wa kimafaniko.

4.Kubaliana na changamoto zinajitokeza.
Tambua ya kuwa hakuna mafanikio yasiyo kuwa na changamoto.Hivyo jitahidi kuwa ni mtu kukubaliana na changamoto hizo na kujua namna utavyoweza kumbana na changamoto.Usiwe ni mtu wa kukata tamaa.Vile vile siri kubwa ya mafanikio ni kujifunza na kutokuogopa kujaribu.Hautaweza kufanikiwa kwa kukaaa tu na kutokuwa mbunifu na jinsi ya kupambana kimaisha na changamoto za kimaisha na hatimaye kufanikiwa.Hakikisha unafanya kazi kwa biidii ili malengo yako yaweze kutimia.

5.Fanya kazi kwa bidii.
Hiyo ni nguzo kubwa katika mafanikio.Hakikisha unajituma zaidi katika kufanya kazi .Tumia muda wako vizuri na kwa mapangalio mzuri ili kuhakikisha unapata mafanikio unayoyahitaji.Tumia ujuzi,nguvu na maarifa uliyonayo katika kufanya kazi.

6.Simamia maono yako.
Hakikisha unasimamia malengo yako uliyojiwekea ili kuona ndoto zako zinatimia kwa muda muafaka.Maono ni malengo yako ambayo wewe mwenyewe umejiwekea ambayo utapenda kuyatimiza hapo baadae na kuona unayaona mafanikio.Kumbuka kufanya tathimini ya malengo yako ni wapi ulishindwa kutimiza malengo yako, na utaweje kukumbana na changamoto hizo na hatimaye kutimiza malengo yako.


Misingi 5 Ya Kuifahamu Kabla Hujaanza Biashara.

Mara nyingi baadhi yetu huwa tunaanza biashara kwa kusikia kwa watu faida ya biashara hiyo, bila kuwa na msingi halisi wa kuifahamu biashara husika.  Lakini katika makala yetu hii ya leo tutaangalia misingi muhimu ya kuielewa mapema kabla ya kuanza biashara yoyote.

Mambo hayo ya msingi tutakayojifunza hapa ni maalumu kwa ajili ya wote wanaotaka kuwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo pia. Kwa yeyote anahitaji kupata faida kubwa na kuepuka kupata hasara zisizo za lazima katika biashara yake, misingi hii ni muhimu sana kwake kuijua.

1. Eneo la kufanyia biashara.
Kwa kuwa ndio kwanza unaanza kufanya biashara lazima ufanye uchunguzi wa kutosha juu ya kile unatochotaka kukifanya. Eneo hili lakufanyia biashara  ni lazima ulichunguze kwa kuangalia uhitaji wa  wa wateja wa eneo husika.

Kwa mfano kama unataka kufanya biashara ya kuuza vifaa vya shule (stationery) lazima ujiulize ni wapi ambako unahisi ukiweka biashara yako kuna wateja wengi. Baada ya kufikiri unaweza ukaangalia kwenye maeneo ya shule,vyuo , kanisani na maeneo mengine.

Lakini hiyo haitoshi nenda sehemu husika jaribu kufanya uchunguzi ni vitu gani wanavifanya wafanyabiashara wengine ambao wana biashara kama yako? Angalia ni changamoto gani wanazozipata ili pindi ukianza kufanya biashara hiyo ujue mbinu za kupambana na changamoto hizo kirahisi.
 
2. Wateja.
Baada ya kuona ni eneo gani linafaa kufanya biashara jambo la pili la kujiuliza je wateja wako watakuwa ni wakina nani? Hili ni swali la msingi sana kujiuliza kwa sababu lengo la kufanya biashara ni kupata wateja wengi, hata hivyo katika kuangalia hili pia fanya uchunguzi wa kina juu mahitaji ya wateja.

Hii utakusadia wewe pindi unapofikiri ni biashara gani ya kufanya.Tukiangalia tena mfano wa kuanziasha biashara ya vifaa vya shule yaani (stationery) tunaona ya kuwa wateja wako watakuwa ni wanafunzi na baadhi ya watu wengine kama eneo ambalo ulilifikiri la kufanyia biashara itakuwa kwenye taasisi yeyote mfano shule au kanisani.

3. Bidhaa.
Ewe msomaji wa makala hii unayependa kufanya biashara yeyote eidha ni ndogo au kubwa lazima ufikiri kwa kina je bidhaa gani ambazo utaziuza? Swali hili la bidhaa utajiuliza baada ya kufanya uchunguzi juu ya eneo husika la kufanyia biashara? na pia kwa kuangalia je ni mahitaji gani ya wateja ?

Pia jifunze kuangalia bidhaa ambazo baada yakufanya  uchunguzi na ukagundua ni bidhaa gani adimu pia zina uhitaji mkubwa chukua kama changamoto na lifanye kama fursa. Ukishapata majibu fanya utaratibu wote mpaka upate bidhaa hizo.
 
4. Matangazo.
Kuna usemi husema biashara matangazo. Hii ni kweli kabisa ili biashara iweze kuwa nzuri ni lazima wateja wako waipate kupitia matangangazo. Matangazo haya yanaweza kuwa kuwajulisha wateja wako juu ya ujio wa bidhaa mpya, mabadiliko ya bei na vitu vinginevyo vihusuvyo biashara.
Matangazo haya unaweza kuyasambaza kupitia mitandao ya jamii na vyombo vya habari pia kwa mfanyabiashara mdogo unaweza ukaandika bango  la biashara nje ya eneo lako la biashara unayoifanyia ili kuwajulisha wateja wako.


Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment