IMANI YAKO............MAFANIKIO YAKO DUNIANI NA AKHERA.

“Sema: Yeye Allaah ni wa pekee. Allaah Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anaye fanana Naye hata mmoja.” (Qur-aan, 112:1-4)
 
Hakuna aliye na haki ya kuombwa, kuelekezewa dua, kuswali kwa ajili yake, au kukusudiwa kwa kila tendo la kiibada, bali Allaah peke Yake.
Allaah peke Yake Ndiye Mwenye enzi, Muumbaji, Mkuu na Mwenye kukiruzuku kila kitu katika ulimwengu wote. Yeye huyaendesha mambo yote. Hana haja kwa yeyote katika viumbe wake, ilhali, viumbe wake wote humhitaji Yeye katika kila walicho na haja nacho. Yeye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona vyote na Mwenye kujua yote. Katika hali ya ukamilifu, ilimu Yake imekizingira kila kitu, cha wazi na cha siri, cha umma na cha binafsi. Anajua kilichotokea, kipi kitatukia na namna kitakavyotukia. Hapana jambo lenye kujiri katika ulimwengu mzima isipokuwa kwa kutaka Kwake. Chochote Akitakacho ndicho na Asichokitaka sicho na kamwe hakitakuwa. Kutaka Kwake kuko juu ya utashi wa viumbe wote. Yeye ana nguvu juu ya vitu vyote, na Anaweza kufanya kila kitu. Yeye ni Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu na Mpaji. Katika mojawapo ya Hadiyth za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), tunaambiwa kwamba Allaah ni Mwenye rehema kwa viumbe wake kuliko mama kwa mwanaye.[73]Allaah Ameepukana mbali dhidi  ya dhuluma na ukandamizaji. Yeye ni Mwenye hikima katika kila Alifanyalo na Analoliamuru. Ikiwa mmojawapo anataka kitu kutoka kwa Allaah, anaweza kumwomba Yeye moja kwa moja, pasi na kumwomba yeyote mwingine amwombe Allaah kwa ajili yake.

Mungu si Yesu, na Yesu si Mungu.[74]Hata Yesu mwenyewe alilikataa hilo. Allaah Anasema katika Qur-aan: “Hakika wamekufuru waliosema: Allaah ni Masihi mwana wa Maryam! Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Allaah, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anayemshirikisha Allaah, hakika Allaah Atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na waliodhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.” (Qur’aan, 5:72)
Mungu si wa utatu. Allaah Anasema katika Qur-aan: “Kwa hakika wamekufuru waliosema: Allaah ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja. Na ikiwa hawaachi hayo wanayoyasema, kwa yakini itawakamata adhabu kali wale wanao kufuru. Je!Hawatubu kwa Allaah na wakamwomba msamaha? Na Allaah ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu. Masihi mwana wa Maryam si chochote ila ni Mtume. Wamekwisha pita Mitume kabla yake. Na mama yake ni mwanamke mkweli. Wote wawili walikuwa wakila chakula. Angalia jinsi tunavyowabainishia Aayah, kisha angalia vipi wanavyogeuzwa.” (Qur-aan, 5:73-75)
Uislamu unakataa kauli kwamba Allaah Alipumzika katika siku ya saba ya uumbaji, kwamba Alishindana mieleka na mmojawapo wa Malaika Wake, kwamba Yeye ni mpangaji njama mwenye husuda dhidi ya mwanaadamu, au kwamba Yeye ni mwenye mwili kwa mwanaadamu yeyote. Kadhalika, Uislamu unakataa kumpa sifa ya Allaah mwanaadamu yeyote. Yote haya yanachukuliwa kuwa ni kufuru. Allaah ni Mtukufu, Ameepukana mbali na kila sifa ya upungufu. Kamwe hapatwi na uchovu. Katu Yeye hashikwi na usingizi wala halali.
Maana ya neno la kiarabu, Allaah, ni Ilahi (Mmoja na Mungu pekee wa kweli Aliyeumba ulimwengu mzima). Neno hili, Allaah, ni jina la Allaah ambalo hutumiwa na wazungumzaji wa lugha ya Kiarabu, wote kwa pamoja, Waarabu ambao ni Waislamu na wakristo. Neno hili haliwezi kutumika kuonesha kitu kingine isipokuwa Mungu mmoja wa kweli. Neno la kiarabu Allaah linatokea zaidi ya mara 2150 katika Qur-aan. Katika lugha ya ki-Aramaic inayokaribiana sana na Kiarabu na lugha ambayo Yesu alipenda kuitumia, Mwenyezi huitwa pia kwa jina, Allaah.
2) Kuwaamini Malaika
Waislamu wanaamini kuwepo kwa Malaika na kwamba wao ni viumbe waliotukuzwa. Malaika humwabudu Allaah tu, humtii na hufanya vile walivyoamrishwa na Mungu tu Miongoni mwa Malaika hao ni Jibriyl, aliyeishusha Qur-aan kwa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
 
3) Kuamini Vitabu Vilivyoteremshwa na Mungu
Waislamu wanaamini kuwa Allaah Aliwateremshia Mitume wake Vitabu kama ushahidi kwa mwanaadamu na mwongozo kwao. Miongoni mwa Vitabu hivyo ni Qur-aan ambacho Allaah Alikiteremsha kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Allaah Ameipa ulinzi Qur-aan dhidi ya uharibifu au upotoshaji wowote. Allaah Amesema: (Qur-aan, 15:19)
4) Kuwaamini Mitume na Wajumbe wa Allaah
Waislamu wanawaamini Mitume na Wajumbe wa Allaah, kuanzia Aadam, pamoja na Nuuh, Ibraahiym, Isma’iyl, Is-haaq, Ya’aquub, Muusa na ‘Iysa (Yesu) (‘Alayhimus Salaam). Lakini, ujumbe wa mwisho wa Allalah kwenda kwa mwanaadamu, uthibitisho wa ujumbe wa milele, ulifunuliwa kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Waislamu wanaamini kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni Mtume wa mwisho aliyetumwa na Allaah sawa na kauli ya Allaah: “Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Allaah na Mwisho wa Manabii...” (Qur-aan, 33:40)
Waislamu wanaamini kuwa Mitume na Manabii wote walikuwa ni wanaadamu ambao hawakuwa na sifa yoyote ya uungu.
 
5) Kuamini Siku ya Hukumu
Waislamu wanaamini Siku ya Hukumu (Siku ya Ufufuo) ambapo watu wote watafufuliwa kwa ajili ya kuhukumiwa na Allaah, kulingana na imani zao na matendo yao.
6) Kuamini Al-Qadar
Waislamu wanaamini Al-Qadar, ambayo ni maamuzi ya Mungu, lakini kuamini hivyo hakumaanishi kuwa wanaadamu hawana khiyari. Vinginevyo, Waislamu wanaamini kuwa Allaah Amewapa wanaadamu khiyari. Hii inamaanisha kuwa wanaweza kuchagua lililo la haki na la makosa na kwamba wanawajibika katika khiyari yao. Imani katika Qadar, inajumuisha kuamini mambo manne:
 
1) Allaah Anajua kila kitu. Anajua kilichotokea na kitakachotokea.
2) Allaah Amekiandika kila kilichotokea na kila kitakachotokea.
3) Chochote Allaah  Atakacho kitokee hutokea, na asichotaka kitokee, hakitokei.
4) Allaah ni Muumbaji wa kila kitu.
Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment