SIASA KATIKA DINI SAWA NA MAJI KWA MAFUTA LAZIMA VITAJITENGA TU

Uislam ni dini ambayo haiwezi kuendeshwa kisiasa na wala huwezi kuinyooka haki kwa kuitegemea batili ... Toka zamani nchi yetu haiko tena chini ya amri za Allah S.W 
Sasa vipi mkae vikao wenyewe kisha mteue wenyewe huku mkisema mnasimamisha haki????

Kweli haitosimama Qiyama mpaka makundi 73 yatimie.

KWA TAARIFA HII ILIYOTOKA    INASABABISHA KUJUA WAZI KUWA DALILI ZA QIYAMA NDO HIZI HAPA.

Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuberi amesema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limefanya mabadiliko ya upatikanaji wa viongozi kwa nchi nzima kuanzia ngazi ya Masheikh wa wilaya, mikoa na Taifa.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati akitoa maazimio ya kikao cha Baraza Kuu la BAKWATA kikao kilichokaa Mjini Dodoma mwishoni mwa mwezi Machi, Mufti amesema wamekubaliana kwa kauli moja kuwa upatikanaji wa viongozi wa Kiislamu utakua ni wakuteuliwa na sio kuchaguliwa tena kama ilivyo sasa.

Amesema Mkutano Mkuu uliofanyika tarehe Machi 31 - Aprili 1 umesema kuwa mfumo wa uchaguzi hauwaachi watu salama sana sana husababisha migogoro ya hapa na pale na makundi yenye kuleta chuki na kwamba mfumo wa kuteua ndiyo mfumo wa kiislam

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA taifa Sheikh Khamis Mataka amesema mbali na utaratibu huo wameanzisha mfumo mmoja wa kukusanya mapato ili kukusanya fedha hizo kwa umakini tofauti na ukusanyaji wa sasa ambao una mapungufu mengi na kupoteza baadhi ya mapato.
Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment