- Chapisha
- Login or register to post comments
- Kutuma Kwa Email
Du'aa Kutoka Qur-aan Na Maana Yake
رَبِّ اجْعَلْ هَـَذَا
بَلَدًا آمِنًا وَارْزُق ْأَهْلَهُ مِنَ الثَّمَرَاتِ مَنْ آمَنَ مِنْهُم
بِاللّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ (البقرة:126)
Ee Mola wangu! Ufanye huu
uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda, wale wanaomuamini Allaah na
Siku ya Mwisho. (Al-Baqarah: 126)
رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ
رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَآ إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ (البقرة
127- 128)
Ewe Mola wetu! Tutakabalie!
Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi.Ewe Mola wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe ummah uliosilimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. (Al-Baqarah: 127-128)).
رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الآخِرَةِ حَسَنَةً
وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ (البقرة 201 )
Mola wetu, tupe duniani
mema, na Aakhirah mema, na utulinde na adhabu ya Moto. (Al-Baqara 201)
رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا
وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ (البقرة 250 )
Mola wetu! Tumiminie subira,
na isimamishe imara miguu yetu, na utusaidie tuwashinde watu Makafiri
(Al-Baqarah: 250)
رَبَّنَا لاَ تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا رَبَّنَا
وَلاَ تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا
رَبَّنَا وَلاَ تُحَمِّلْنَا مَا لاَ طَاقَةَ لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ
لَنَا وَارْحَمْنَا أَنتَ مَوْلاَنَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ
الْكَافِرِينَ (البقرة 286)
Mola wetu! Usituchukulie
tukisahau au tukikosea. Mola wetu! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale
walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Usitutwike tusiyoyaweza, na utusamehe, na
utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde
kaumu ya makafiri. (Al-Baqarah: 286)
رَبَّنَا لاَ تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا
مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ (آل عمران 8 )
Mola wetu! Usizipotoe nyoyo
zetu baada ya kwishatuongoa, na utupe rehema itokayo kwako. Hakika Wewe ndiye
Mpaji. (Al-'Imraan: 8)
رَبَّنَا إِنَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ
النَّارِ (آل عمران 16)
Mola wetu! Hakika sisi
tumeamini, basi tufutie madhambi yetu, na tuepushe na adhabu ya Moto.
(Al-Imran 16)
رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنْكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً إِنَّكَ سَمِيعُ
الدُّعَاء (آل عمران 38]
Mola wangu! Nipe kutoka
kwako uzao mwema. Wewe ndiye unayesikia maombi. (Al-'Imraan: 38)
رَبَّنَا آمَنَّا بِمَا أَنزَلَتْ وَاتَّبَعْنَا الرَّسُولَ
فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ (آل عمران
53)
Mola wetu! Tumeyaamini
uliyoyateremsha, na tumemfuata huyu Mtume, basi tuandike pamoja na
wanaoshuhudia. (Al-'Imraan: 53)
ربَّنَا اغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسْرَافَنَا فِي أَمْرِنَا
وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَِ (آل عمران 147)
Mola wetu! Tughufirie
madhambi yetu na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu, na isimamishe imara
miguu yetu na utunusuru tuwashinde kaumu ya makafiri (Al-'Imraan: 147)
رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَذا بَاطِلاً سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ
النَّارِ رَبَّنَا إِنَّكَ مَن تُدْخِلِ النَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُ وَمَا
لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ رَّبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِيًا يُنَادِي
لِلإِيمَانِ أَنْ آمِنُواْ بِرَبِّكُمْ فَآمَنَّا رَبَّنَا فَاغْفِرْ لَنَا
ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّئَاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ الأبْرَارِ رَبَّنَا
وَآتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَى رُسُلِكَ وَلاَ تُخْزِنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ
إِنَّكَ لاَ تُخْلِفُ الْمِيعَاد ِ
(آل عمران
191-194)
Mola wetu! Hukuviumba hivi
bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto. Mola wetu! Hakika unaye mtia Motoni umemhizi; na waliodhulumu hawana wasaidizi.
Mola wetu! Hakika sisi tumemsikia mwenye kuita akiitia Imani kwamba: Muaminini Mola wenu; nasi tukaamini. Basi tusamehe madhambi yetu, na utufutie makosa yetu, na utufishe pamoja na watu wema.
Mola wetu! Na utupe uliyotuahidi kwa Mitume wako, wala usituhizi Siku ya Qiyaamah. Hakika Wewe huvunji miadi. (Al-'Imraan :191-194)
رَبَّنَا
أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا (النساء:75)
Mola wetu! Tutoe katika mji
huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anayetoka kwako,
na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako. (An-Nisaa: 75)
رَبَّنَا آمَنَّا فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ (المائدة:83)
Mola wetu! Tumeamini. Basi
tuandike pamoja na wanaoshuhudia (Al-Maaidah: 83)
رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا
وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ (الأعراف23)
Mola wetu! tumejidhulumu
nafsi zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye
kukhasirika (Al-A'raaf: 23)
رَبَّنَا لاَ تَجْعَلْنَا مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ (الأعراف 47)
Mola wetu! Usitujaalie kuwa
pamoja na watu waliodhulumu (Al-A'raaf: 47)
رَبَّنَا افْتَحْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمِنَا بِالْحَقِّ وَأَنتَ
خَيْرُ الْفَاتِحِينَ (الأعراف:89)
Ewe Mola wetu! Tuhukumie
baina yetu na kaumu yetu kwa haki, nawe ndiye mbora wa wanaohukumu.
(Al-A'raaf: 89)
رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَتَوَفَّنَا مُسْلِمِينَ ( الأعراف 126)
Ewe Mola wetu! Tumiminie
uvumilivu na utufishe hali ni Waislamu. (Al-A'raaf: 126)
أَنتَ وَلِيُّنَا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا وَأَنتَ خَيْرُ
الْغَافِرِينَ (الأعراف 155)
Wewe ndiye Rafiki Mlinzi
wetu. Basi tughufirie na uturehemu. Na Wewe ndiye mbora wa kughufiria (Al-A'raaf: 155)
حَسْبِيَ اللّهُ لا إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَهُوَ
رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ (التوبة 129)
Allaah ananitosheleza.
Hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye tu. Mimi namtegemea Yeye, na
Yeye ndiye Mola wa 'Arsh tukufu. (At-Tawbah: 129)
رَبَّنَا لاَ تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ
وَنَجِّنَا بِرَحْمَتِكَ مِنَ الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ (يونس85-86)
Ewe Mola wetu! Usitufanye
wenye kutiwa misukosuko na hao watu madhaalimu. Na utuokoe kwa rehema yako na watu makafiri (Yuwnus: 85 – 86 )
رَبِّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ أَنْ أَسْأَلَكَ مَا لَيْسَ لِي بِهِ
عِلْمٌ وَإِلاَّ تَغْفِرْ لِي وَتَرْحَمْنِي أَكُن مِّنَ الْخَاسِرِينَ (هود 74)
Ewe Mola wangu! Mimi
najikinga kwako nisikuombe nisio na ujuzi nalo. Na kama hunisamehe na
ukanirehemu, nitakuwa katika waliopata khasara. (Huwd: 47)
رَبِّ اجْعَلْنِي مُقِيمَ الصَّلاَةِ وَمِن ذُرِّيَّتِي رَبَّنَا
وَتَقَبَّلْ دُعَاء (إبرهيم-40)
Mola wangu! Nijaalie niwe
mwenye kusimamisha Swalaah, na katika dhuriya zangu pia. Ewe Mola wetu, na
ipokee dua yangu. (Ibraahiym: 40)
رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ
يَقُومُ الْحِسَاب (إبرهيم41 )
Mola wetu! Unighufirie mimi
na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya kusimama hisabu. (Ibraahiym:
41)
أَنتَ وَلِيِّي فِي الدُّنُيَا وَالآخِرَةِ تَوَفَّنِي مُسْلِمًا وَأَلْحِقْنِي
بِالصَّالِحِينَ (يوسف:101)
Wewe ndiye Mlinzi wangu
katika dunia na Aakhirah. Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu na nichanganyishe na
watendao mema. (Yuwsuf: 101)
رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا (الإسراء 24)
Mola wangu! Warehemu kama
walivyo nilea utotoni. (Al-Israa: 24)
رَّبِّ
أَدْخِلْنِي مُدْخَلَ صِدْقٍ وَأَخْرِجْنِي مُخْرَجَ صِدْقٍ وَاجْعَل لِّي مِن
لَّدُنكَ سُلْطَانًا نَّصِيرًا (الإسراء-80)
Mola wangu! Niingize
muingizo mwema, na unitoe kutoka kwema. Na unipe nguvu zinazo toka kwako
zinisaidie. (Al-Israa: 80)
رَبَّنَا آتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً وَهَيِّئْ لَنَا مِنْ
أَمْرِنَا رَشَدًا (الكهف10)
Mola wetu! Tupe rehema
itokayo kwako, na tutengezee uongofu katika jambo letu. (Al-Kahf: 10)
رَبِّ اشْرَحْ لِي صَدْرِي وَيَسِّرْ لِي أَمْرِي
وَاحْلُلْ عُقْدَةً مِّن لِّسَانِي يَفْقَهُوا قَوْلِي (طه 25-28)
Ewe Mola wangu! Nikunjulie
kifua changu,Na unifanyie nyepesi kazi yangu,
Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu. (Twaahaa: 25-28)
رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا (طه 114)
Mola wangu! Nizidishie
ilimu. (Twaahaa: 114)
لا إِلَهَ إِلا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ
الظَّالِمِينَ (الأنبياء87)
Hapana mabudiwa wa
haki isipokuwa Wewe Subhaanaka Uliyetakasika. Hakika mimi nilikuwa
miongoni mwa wenye kudhulumu. (Al-Anbiyaa: 87)
رَبِّ لاَ تَذَرْنِي فَرْدًا وَأَنتَ خَيْرُ
الْوَارِثِينَ (الأنبياء 89 )
Mola wangu! Usiniache peke
yangu, na Wewe ndiye Mbora wa wanaorithi (Al-Anbiyaa: 89)
رَبِّ أَنْزِلْنِي مُنْزَلاً مُبَارَكاً وَأَنْتَ خَيْرُ الْمُنْزِلِينَ (المؤمنون 29)
Mola wangu! Niteremshe
mteremsho wenye baraka, na Wewe ni Mbora wa wateremshaji (Al-Mu'minuwn 29)
رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ وَأَعُوذُ بِكَ
رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ (المؤمنون97-98)
Mola wangu! Najikinga kwako
na wasiwasi wa mashet'ani. Na najikinga kwako, Mola wangu, wasinikaribie.
(Muuminuwn: 97-98)
رَبَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا وَأَنتَ خَيْرُ
الرَّاحِمِينَ (المؤمنون 109)
Mola wetu! Tumeamini; basi
tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe Mbora wa wanaorehemu. (Muuminuwn: 109)
رَّبِّ اغْفِرْ وَارْحَمْ وَأَنتَ خَيْرُ الرَّاحِمِينَ (المؤمنون 118)
Mola wangu! Samehe na
urehemu nawe ni Mbora wa wanaorehemu (Al-Muuminuwn: 118)
رَبِّ هَبْ لِي حُكْماً وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ
وَاجْعَلْ لِي لِسَانَ صِدْقٍ فِي الأَخِرِين
وَاجْعَلْنِي
مِنْ وَرَثَةِ جَنَّةِ النَّعِيمِ (الشعراء
83-85)
Mola wangu! Nitunukie hukumu
na uniunganishe na watendao mema. Na unijaalie nitajwe kwa wema na watu watakao
kuja baadaye. Na unijaalie katika warithi wa
Bustani za neema. (Ash-Shu'araa: 83-85)
رَبِّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي
(القصص 16)
Mola wangu! Hakika mimi
nimejidhulumu nafsi yangu; basi nisamehe (Al-Qaswas: 16)
رَبِّ بِمَا أَنْعَمْتَ عَلَيَّ فَلَنْ أَكُونَ ظَهِيرًا لِلْمُجْرِمِينَ (القصص 17)
Mola wangu! Kwa
ulivyonineemesha, basi mimi sitokuwa kabisa msaidizi wa wakosefu (Al-Qaswas:
17)
رَبِّ نَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ (القصص 21)
Mola wangu! Niokoe na watu
madhaalimu. (Al-Qaswas: 21)
رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَاماً ) الفرقان
65
)
Mola wetu! Tuondolee adhabu
ya Jahannam. Hakika adhabu yake ikimpata mtu haimwachi (Al-Furqan 65)
رَبَّنَا
هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَاماً (الفرقان 74)
Mola wetu! Tupe katika wake
zetu na wetoto wetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wachaji
Allaah. (Al-Furqaan: 74)
رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَى وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحاً
تَرْضَاهُ وَأَدْخِلْنِي بِرَحْمَتِكَ فِي عِبَادِكَ الصَّالِحِينَ (النمل 19)
Ee Mola wangu! Nizindue
niishukuru neema yako uliyonineemesha mimi na wazazi wangu, na nipate kutenda
mema uyapendayo, na uniingize kwa rehema yako katika waja wako wema. (An-Naml:
19)
وَأُفَوِّضُ أَمْرِي إِلَى اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ (غافر 44)
Nami namkabidhi Allaah mambo
yangu. Hakika Allaah Anawaona waja wake.(Ghaafir: 44)
رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَى وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَصْلِحْ لِي
فِي ذُرِّيَّتِي إِنِّي تُبْتُ إِلَيْكَ وَإِنِّي مِنْ الْمُسْلِمِينَ (الأحقاف 15)
Mola wangu! Niwezeshe
nishukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema
unayo yapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na
mimi ni miongoni mwa Waislamu. (Al-Ahqaaf: 15)
رَبَّنَا اكْشِفْ عَنَّا الْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ (الدخان 12)
Mola wetu!
Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini. (Ad-Dukhaan: 12)
رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا
الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالإِيمَانِ وَلاَ
تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَؤُوفٌ رَّحِيمٌ (الحشر
10)
Mola wetu! Tughufirie sisi
na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu
undani kwa walioamini. Mola wetu! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu.
(Al-Hashr: 10)
رَّبَّنَا
عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ
رَبَّنَا لاَ تَجْعَلْنَا فِتْنَةً
لِّلَّذِينَ كَفَرُوا وَاغْفِرْ لَنَا رَبَّنَا إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (الممتحنة 4-5)
Mola wetu! Juu yako
tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndio marejeo. Mola wetu! Usitufanyie mtihani kwa waliokufuru. Na tusamehe, Mola wetu. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. (Al-Mumtahina: 4 -5 )
رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا إِنَّكَ عَلَى
كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (التحريم 8)
Mola wetu! Tutimilizie nuru
yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu .(At-Tahriym: 8)
رَبِّ
اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيْتِيَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَلَا تَزِدِ
الظَّالِمِينَ إِلَّا تَبَارًا) نوح:28)
Mola wangu! Nighufirie mimi
na wazazi wangu, na kila aliyeingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na
Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. Na wala usiwazidishie walio dhulumu
ila kupotea. (Nuwh: 28)
0 comments:
Post a Comment