UTAPIGWA MAWE MTI WA MATUNDA (ISLAMIC)




Illuminati sio neno geni kwa wengi wetu. Hata hivyo sio wengi tunao-elewa malengo ya Illuminati. Bila kujua malengo ya Illuminati, sio rahisi kuona mantiki wa yale yanatokea katika Ulimwenguni wetu au dunia kila siku.Ukijua malengo yao, utaelewa maana halisi wa yale yanayotokea katika Ulimwengu unaokuzunguka.

Lakini hasa Illuminati ni akina nani?

Illuminati ni kikundi cha watu wenye ufahamu zaidi ya wengine au kikundi kinachodai kwamba kina ufahamu zaidi ya watu wengine. Kikundi hiki kinaundwa na familia 13 na ndicho kinachodhibiti vikundi vingine vyote vya siri duniani kagma Freemasons, Skull and Bones, Jesuits nk.

Kikundi hiki kama nilivyotangulia kusema kina malengo kwa dunia na Ulimwengu kwa ujumla. Malengo hayo yako 22 na ni kama ifuatavyo:

1. Kuvibadili vitabu vilivyokuwa mwongozo sahihi kwa mwanadamu vikiwemo, TAURATI (aliyokuja nayo Nabii MUSA), ZABURI (Ibrahimu), INJILI (nabii ISA/ YESU). Kwa kuwa vitabu hivyo vilikuwa vinazungumza wazi wazi ka haikupatikana shaka ndani yake" Hivyo waliona itakuwa ngumu kwao kueneza ukafili wao ndipo walipo kaa kikao na kuamua kuyabadili mambo yote yaliyokuwa kwenye vitabu hivyo na kukiunda kitabu kimoja HOLY BIBLE na mpaka sasa wanajitahidi nchi zote hapa duniani zinatafsiliwa hiyo HOLY BIBLE kwa Lugha yao ili ukafili wao uenee katika mataifa yoteeeeeeeeeee. 
Ila MUNGU aliyajua yote ndipo alipoamua kuileta Q'URAN inayowatangaza wazi wazi hao FREE MASONS.

2.Kuunda serikali moja ya dunia au Mfumo Mpya wa Dunia (New World Order-NWO) wenye Kanisa moja na mfumo mmoja wa kifedha. Serikali hiyo moja ya dunia ilianza kuunda kanisa hilo miaka ya kati ya 1920 na 1930 kwa sababu walitambua umuhimu wa imani kwa mwanadamu na haja ya kuwa na chombo ambacho wanadamu wataweza kuelekeza imani hiyo, lakini katika mfumo ambao wao Illuminati wanataka.

3.Kuharibu kabisa utaifa. Hii waliona ni muhimu ili kuweza kufanikisha nia ya kuwa na serikali moja ya dunia.

4.Kuharibu mifumo yote ya dini, hasa dini ya Kikristo, isipokuwa ile ambayo wameunda wao kama ilivyoelezwa hapo juu.

5.Kuunda mfumo wa kuweza kumdhibiti kila mtu kwa kutumia tekinolojia za kudhibiti ubongo kama RFID. Mpango huu utatengeneza wanadamu walio kama maroboti.

6.Kusitisha mifumo yote ya viwanda na utengenezwaji wa umeme wa nuclear katika kile wanachoita "Jamii isiyokuwa na ukuaji wa viwanda kabisa yaani "post zero industrial growth society."Viwanda ambavyo vitaruhusiwa kuendelea ni vya kompyuta na vya kutoa huduma tu. Viwanda vitakavyobaki vitahamishiwa maeneo ambako nguvu kazi nyingi ya "watumwa"inapatikana kama Mexico. Kama tulivyo-ona mwaka 1993, hii imetokea kupitia kwenye kuidhinishwa kwa North Amercan Free Trade Agreement au NAFTA. Watu ambao hawataweza kuajiriwa baada ya kuharibu mifumo ya viwanda, watafanywa kuwa watumiaji wa madawa ya kulevya kama opium, heroin au cocaine na hatimaye wataingizwa kwenye idadi ya watu watakaondolewa kama watu wasiohitajika kama ilivyoainishwa kwenye "Global 2000 report."

7.Kuhamasisha na hatimaye kuhalalisha matumizi ya madawa ya kulevya na kufanya uangaliaji wa picha za ngono iwe sanaa, ambayo hatimaye itakubalika na jamii na kuwa kitu cha kawaida.

8.Kupunguza idadi ya watu duniani katika miji mikubwa kwa kufuata misingi ile iliyotumika wakati wa Pol Pot kule Cambodia. Inashangaza kuona kwamba mipango ya mauaji aliyotumia Pol Pot ilibuniwa Marekani na kikundi cha The Club of Rome na kusimamiwa na Thomas Enders,Afisa wa juu kabisa wa The State Department.

9.Kukandamiza maendeleo yote ya kisayansi isipokuwa
yale yenye manufaa kwa Illuminati. Mkazo mkubwa utakuwa kwenye nguvu za nuclear kwa sababu za kijamii. Maendeleo ya tekinolojia ya Fusio Torch ambayo inatumia maliasili za kawaida na kidogo kwa kupata nishati.
hazitaruhusiwa kabisa kwa kuwa hizi zina faida kubwa kwa wanadamu. Tekinolojia hii ingewawezesha wanadamu kupata nishati hata milele bila kuharibu mazingira kabisa.

10.Kupunguza watu kwa vita vya hapa na pale katika nchi zilizoendelea na njaa na magonjwa katika nchi za dunia ya tatu, wapatao billioni tatu ifikapo mwaka 2050 ya watu wanaowaita"Walaji wasio na faida- Useless Eaters". Kamati yao ya watu 300 ilimpa Cyrus Vance kuandika ripoti ya jinsi mauaji haya yatakavyofanyika. Ripoti hii ililetwa katika kile kinachoitwa "Global 200 Report."Report hii ilikubaliwa na kupitishwa na Rais James Earl Carter na Secretary of State Edwin Muskie kwa niaba ya serikali ya Marekani.

11.Kudhoofisha mifumo ya maadili mema kwa wanadamu katika mataifa yote na kukatisha tamaa nguvu kazi kwa kuwakosesha ajira. Ajira zinapokosekana kwa kukosekana viwanda kwa sababu ya sera mbovu zilizoletwa na The Club of Rome, Illuminati wanaamini nguvu kazi hiyo itageukia unywaji pombe na madawa ya kulevya. Vijana pia watashawishiwa kwa kutumia Muziki wa Rock au siku hizi hapa kwetu Bongo Flava, kuiasi mamlaka na hatimaye kuharibu misingi ya familia.

12.Kuwafanya watu kila mahali wasiweze kuamua hatima ya maisha yao kwa kuwaletea tatizo au janga moja baada ya jingine halafu kujifanya kushuhulikia majanga hayo au matatizo hayo. Hii itawachanganya watu kiasi kwamba kwa sababu ya majanga na matatizo mengi watakata tamaa na kuona kwamba maisha hayana thamani kabisa na hivyo kuwa rahisi kutawala na kuyumbisha. (Tafakari uongozi ulipo sasa katika nyanja za uongozi katika nchi yako)

13.Kuunda vikundi vingi vya imani potofu na kuendelea kuunga mkono vile vilivyopo kama vya Muziki wa Rock kwa mfano Tanzania na vikundi vya Bongo Flava.

14.Kuendelea kujenga vikundi vya imani kali za Kikristo ambavyo vilianzishwa kwa mara ya kwanza enzi za British East India Company. Vikundi hivi vitatumika kujenga Taifa la Kizayuni la Israel kwa kutumia filosofia ya "Taifa Teule la Mungu" kwa kulipelekea michango na misaada mbalimbali" kwa imani kwamba kufanya hivyo ni tendo la Kikristo!

15.Kuendelea kuhimiza kuenea kwa vikundi vya imani potofu kama The Moslem Brotherhood, Al Shabab, Mujahedin, ISIS nk. na kuendelea kuyafanya majaribio ya kudhibiti akili za Wanadamu. Ni muhimu kutambua kwamba Marehemu Khomeini ni matunda ya idara ya Kijasusi ya Uingereza MI6 (British Military Intelligence Division 6).

16.Kusambaza mawazo ya uundwaji wa vikundi visivyokuwa chini ya mamlaka ya madhehebu ya asili duniani, kama Ministries, hasa kwenye madhehebu ya Kikrito. Dhana hii itachangia kubomoa mamlaka na ushawishi wa
makanisa hayo kwa waumini wao.

17.Kuharibu kabisa mifumo ya uchumi wa dunia na siasa.

18.Kutawala mifumo ya siasa za nchi nje na ndani ya nchi ya Marekani na dunia kwa ujumla.

19.Kuunga mkono kwa nguvu zote mashirika makubwa ya dunia kama Umoja wa Mataifa (UN), Shirika la Fedha Duniani (IMF), The Bank of International Settlements, Koti ya Dunia (The World Court) na kila inapowezekana kuzifanya taasisi za nchi moja moja zisiwe na nguvu na hatimaye kuzifanya ziwe chini ya Umoja wa Matsifa.

20.Kuzihujumu serikali za dunia na hatimaye kuzifanya zisiwe na mamlaka kama nchi.

21.Kuunda mfumo wa kigaidi wa dunia.

22.Kuudhibiti mfumo wa elimu wa Marekani na dunia kwa ujumla kwa nia ya kuuharibu kabisa.

Nimejitahidi kutafsiri kwa Kiswahili kwa wale ambao hawajui Kingereza.Hata hivyo zipo sehemu chache ambazo nimeziacha kwa kuwa sikupata maneno mazuri ya Kiswahili. Naomba msamaha kwa hili.

Kwa wale wakali wa Kimombo,naomba mfuate hii link, www.theforbiddenknowledge.com/hardtruth/targets_of_illuminati.htm au google,"Targets of The Illuminati &The Committee of 300."
TAMBUE MAANA YA FREEMASONS,ALAMA ZAKE NA MADHUMUNI YAKE.....SEHEMU YA 1


Seebait.com 2016SeeBait
                                      UTANGULIZI
Yapo mambo mengi sana duniani ambayo huja na kupita.mengi huwa tunayaona mageni pale tunapo yaona kwa mara ya kwanza.mfano vazi la suruali kwa wanawake. 

Vazi hili miaka ya 80 halikuwepo hapa kwetu tanzania.miaka ya 90 vazi hili lilianza kutumika japo watumiaji walipata vipingamizi vingi sana kama kubakwa,kuzomewa,kutengwa, nk.watu hao walionekana katika jamii kama wasaliti wa mila.hata hivyo mpaka sasa jamii imekwisha kubali matokeo.

                               HISTORIA KWA UFUPI

Freemason  ni shirika ambalo mambo yake ni siri kuu. Mimi nilifanya utafiki  kwenye mitandao, nikafatilia historia yao kama inavyoonyeshwa mara kwa mara kwenye makala za historia katika televisheni za magharibi pamoja na kuongea na watu waliofuatilia kwa karibu mambo yao.

Kwenye maelezo yao kwa nje Free masons wanajitangaza kama shirika zuri tu.
Naomba niorodheshe mambo machache niliyoambiwa kuhusiana na Freemasonry.

1. Ni kweli Freemasonry kama ilivyo maana yake kwanza ilkuwa ni kundi la mafundi waashi (masons) au wajenzi kuwa lugha nyingine. Walikuwa ni wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki ya zama hizo zinazoitwa kwa kizungu (medieval times). 

Niliambiwa walikuwa ni watunzaji wa pesa za kanisa katoliki. Kwani walikuwa wanajenga mahekalu(cathedrals) za wakatoliki na mabenki/ mahandaki ya kuhifadhia pesa pamoja na kuzikia(catacombs). 

Niliambiwa wanaweza kujenga hayo maandaki kwa utaalamu mkubwa kiasi kwamba ukiingia ndani ya hayo mahandaki bila ramani unaweza ukashindwa kutoka hata unaweza kupotelea humo humo ndani usiweze kutoka tena. Hicho ndicho kilichokuwa ni kiwango cha utaalamu wao.

2. Kwa kuwa walikuwa ni waashi ndiyo maana alama zao ni vifaa vya ujenzi, Pima maji n.k

3. Inasemekana mji mkuu wa marekani (Washington DC) ulisanifiwa na kujengwa na Freemasons. Na inasemekana ni mji makini ambao umejengwa ukizingatia pembe tatu zenye nyuzi zinazowakilisha u freemason.

3. Ikatokea kipindi ambapo hawa freemasons wakaasi kwa kuanza kujishirikisha na mambo ya nguvu za giza. Wengine wanasema walianza kuiba pesa za kanisa katoliki, lakini ukweli halisi haujulikani. Kutokana na sababu hizi na zinginezo ambazo ni siri kati ya kanisa katoliki na freemasons, Freemasons wakafukuzwa kutoka ukatoliki. 

Ndio maana hakuna maelewano kati ya freemasons na wakatoliki. Wakatoliki wakaanzisha shirika jingine badala ya hao freemasons lijulikanalo kama Jesuits.

Jesuit Fathers ni mapadri wa katoliki wa daraja la juu sana wenye elimu ya juu zaidi ambao hufanya kazi za siri za utawala na udhibiti ndani ya kanisa katoliki.

4.Kuhusu imani yao (freemasons) nikaelezwa kwa kifupi kuwa wanaamini Yesu na Lucifer ni mtu na ndugu yake. wanaamini kuwa Lucifer ndiye mwema na mzuri lakini wanaamini kuwa Yesu ndiye mwenye mabaya. alimfanyia hila Lucifer aonekane mbaya.

4.Kinachoendelea ndani yake kuhusiana na ibada zake ni siri kwani kuna daraja ambazo muumini wa freemason anapanda kutokana na kubobea katika imani ikiwa ni pamoja na kutunza siri zao. Ninajua kuwa daraja ya juu kabisa ni nyuzi ya 33 (33rd degree)

5. Kwa hiyo ijapokuwa wanatumia biblia wanapoongelea “Bwana” huwa hawamaanishi Yesu bali huwa wanamaanisha Lucifer ambaye ndiye wanayemwabudu.

6. Ni watu wenye nguvu mno na mambo yao ni makubwa mno na siri zao ni nzito mno. Ndiyo maana haziko wazi. 

Wafuasi wa kiwango cha chini wala hawajui shirika hili linahusika na nini manake hata wao hawaambiwi kitu. Kwa wafuasi wa daraja ya chini wanakwenda ku socialize tu. Yaani kwa wasio jua kitu kule kwenye lodge zao ni kama ywca au wmca au club hivi. Kwenye nchi kama marekani watu wasio jua siri wanachukulia kama sehemu za kusocialize tu.

7. Freemasonry inawekwa pamoja na makundi mengine makubwa ya siri, yanayoendesha ulimwengu mzima kwa nguvu za kiuchumi, siasa na mambo ya utawala.


WALIOSHIRIKI KUPINGA  FREEMASON NA UASI WA
LIONS CLUB NA ROTERY CLUB

Kanisa la Katholiki wakati moja waliwahusisha Rotarians (Lions Club) moja kwa moja na Freemasons. Mwaka wa 1928 Maaskofu wa kihispania walitangaza wazi kwamba Rotary Club si chama tu cha kawaida bali ni Muungano au chama kipya cha kuabudu mashetani wakiwa na katiba, tabia na kila kitu chao kufanana na zile za Freemasons wakawatahadharisha waumini wao wajichunge sana na Chama hicho, na baada ya muda mfupi wakuu wa Vatican walitoa amri kwamba maaskofu wa kanisa la katoliki hawaruhusiwi kujiunga na vyama hivyo (Rotary, Lions Club).

Mohammed Sayed Tantawi

Katika miaka ya 1970 kiongozi wa juu na Sheikh wa Chuo kikuu cha kiisilamu huko Misri (Egypt) inasemekana alitoa fatwa kuwakataza waisilamu wasijiunge na chama cha Rotary Club na wakati mambo haya yalikua yakikatazwa na dhehebu la sunni Chama cha rotary pia kilisikika kukatazwa na Ayatollah Khomeini. 

Ayatollah Khomeini

katika mwaka wa 1798 Mwandishi Mmoja wa Kiingereza aliejulikana kwa jina la john Robbinson aliandika kitabu kijulikanacho kama Proofs of a Conspiracy Against All the Religions and Governments of Europe, Carried On in the Secret Meetings of Free Masons, Illuminati, and Reading Societies (Uthibitisho wa njama dhidi ya Dini zote na Serikali zote za Ulaya ilipangwa katika mikutano ya siri ya Freemasons, Illuminati, na vyama vinginevyo vya Reading)
John Robbinson

Kitabu hicho kinaelezea Ari na hamasa za Freemason walivyokuwa wakipanga kisiri jinsi ya kupinduwa mipangilio mizuri ya Maisha (Serikali) na ndio waliosababisha mapinduzi nchini Marekani na Ufaransa.

Shuku za kuenea kwa Freemasons zilienea hadi kufikia miaka ya 1800 ambapo 
Rais Wa 13 Millard Fillmore wa Marekani
alichaguliwa kwa mara ya kwanza katika bunge la Marekani (Congress) kama mgombea aliyekuwa akipinga mambo ya Freemasons na akafikia kilele katika karne ya 20 (20th Century)

Sergiei Nilus Mwandishi Kitabu cha Protocol

Kitabu cha The Protocols of the Elders of Zion sio kuhusu mayahudi kutawala dunia lakini ni kuhusu njama za freemason wa kiyahudi kubadili mfumo wa dunia.

Hitler Reinhard Heydrich

Hitler alizungumzia kuhusu njama za Mayahudi-Bolshevik-Freemason na kiongozi mwingine wa Ujerumani kwa jina la Reinhard Heydrich aliunda kikosi maalum (Special Section SS) kuangamiza ushawishi wa freemason nchini Ujerumani.

Moqtada al-Sadr Al Hawza

Nchini Irak, Gazeti la Moqtada al-Sadr lijulikanalo kama Al Hawza lilichapisha picha ya George H.W. Bush na Bill Clinton na akaelezea kwamba ishara ya mikono yao ilikuwa ni alama ya waandamizi wa kizayoni na freemason, na kama walivyo Wakatoliki Waisilamu pia waliwahusisha wanchama wa Rotary moja kwa moja na Freemasons na kusema vyama vyote viwili ni laana. 

Rais Bush Rais Clinton

Freemasons wamehusika moja kwa moja katika jitihada za kutawala Mashariki ya kati jitahada ambazo zilibuni uhasama kati ya Mashariki ya Kati na Jumuiya ya Magharibi.
Freemason walitoa fursa ya wafanyabiashara kuunda mtandao mmoja, hii ni katika malengo ya wafanyabiashara wanachama wa Freemason wa Ulaya wafungue ofisi za Freemason nje ya nchi na kuwaalika wanainchi wa Ulaya kujiunga nao.

Kwa ujumla sio Wafanya biashara wa Wakiingereza au Mashariki ya kati ndio waliowengi tu kama anavyoeleza bwana Hamid Algar wa Berkeley ambaye ni Mwanachuoni maarufu duniani wa historia ya Kiisilamu:-

Hamid Algar

Freemason imeweza kuhudumika katika uisilamu tangu kijitambulisha kwa waisilamu katika karne ya 18 kama njia ya kukuza utawala wa fikra za wa Magharibi kisiasa na kimawazo; Mojawapo wa Ofisi za Freemason huko Istambul nchini Uturuki, ilikuwa na Balozi wa Uingereza kama mkuu


TUKUTANE KATIKA  SEHEMU YA PILI YA SIMULIZI HILI.,
ASANTENI.


Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment