Inauma sana jamani""Huko Dallas Marekani vitabu vya Qur'an vyakutwa katika vyoo

Baada ya kuwepo na dhuluma nyingi na kashifa nyingi za kuudhalilisha Uislam hapa duniani sasa Nchini Marekani polisi wameanza uchunguzi baada ya nakala za Qur'n kupatikana ndani ya vyoo katika jumba moja la chuo kikuu cha Texas huko Dallas huko nchini Marekani.
Picha kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha vitabu hivyo vikiwa ndani ya vyoo katika jumba moja la chuo kikuu cha Texas huko Dallas huko nchini Marekani..
Polisi wa chuo wanasema kesi hiyo ni ya kushangaza sana na "isiyo ya kawaida" kwani chuo hicho kina wanafunzi kutoka makabila na dini mbali mbali na wameshitushwa na tukio hilo.
Polisi wanajaribu kumtambua mmoja kati ya watu sita walioonekana wakiingia chooni wakati wa tukio hilo la tarehe 28 mwezi wa Machi. Wachunguzi wamekuwa wakikagua video za CCTV wakiwatafuta waliohusika na tukio hilo .
 Mbali na hayo hakuna kitu kilichoguswa katika chumba kimoja ambacho huwa na vitabu vya dini tofauti, kulingana na wachunguzi.
Mkuu wa polisi Larry Zacharias aliiambia Dallas Morning News: "Hakuna anayemjua mmiliki wa vitabu hivyo."
Mohammad Syed ambaye ni rais wa chama cha wanafunzi wa Kiislamu chuoni pia taarifa hizi zilimfikia na mpaka sasa inauma kuona jambo hili linafanywa kuwa la kawaida sana.
Licha ya kuwa kuna idadi kubwa ya wale wenye chuki juu ya dini ya  Kiislam, kuna idadi ndogo  ya upendo kwa wale wasio kuwa waislam wa dini hi.
Qur'an hizo ziligunduliwa na viongozi wa wanafunzi baada ya mkutano wao jioni hiyo uliokuwa unafanyika hapo chuoni.
Jonathan Schuler, aliyepata vitabu hivyo takatifu katika vyoo aliweza kusisitiza wasakamwe walio tenda tendo hilo.
Huu ni mchezo mbaya ambao unazidi kuchochea chuki kwa dini ya Kiislam maana haiwezekani vitabu vipatikane alafu eti walio vitia chooni hawapatikani. Huu ni mchezo wa kuudhalilisha Uislam na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuyajua yote mnayo yaficha au kuyabainisha.
Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

1 comments:

  1. Baada ya kuwepo na dhuluma nyingi na kashifa nyingi za kuudhalilisha Uislam hapa duniani sasa Nchini Marekani polisi wameanza uchunguzi baada ya nakala za Qur'n kupatikana ndani ya vyoo katika jumba moja la chuo kikuu cha Texas huko Dallas huko nchini Marekani.

    ReplyDelete