JE' UNAKIJUA KIPAJI CHAKO!?


Moja ya changamoto kubwa inayowakabili watu wengi ni kutojua kwa undani kipi  kipaji chako ambacho Mungu amekumpa ambacho unaweza ukakitumia kwa namna moja ama nyingine ili uweze kuleta mabadiliko chanya katika jamii na wewe binafsi. NA kwa kuwa kuna watu wengi ndio wapo kundi hilo, kuna usemi unasema ya kwamba wengi wape basi ngoja nifanye hivyo kuweza kuwapa somo hilo la namna ya kujua kipaji chako  kwani hii itamsadia kila mmoja ambaye atakwenda kufuatana nami mwanzo hadi mwisho katika mukutadha wa makala haya. 

Tunapozungumzia neno kipaji huenda kila mmoja akawa na maana yake ambayo anaifahamu, lakini kwa namna moja ama nyingine ni lazima mtu aweze kuzaliwa nacho hivyo Mwenyezi Mungu husika pia katika kumpa mtu kipaji. Hivyo endapo mtu atakifahamu kipaji chake inampasa sasa ajue namna ya kukiendeleza kipaji hicho ili kisife. Pia ikumbukwe ya kwamba tunapozungumzia kipaji tunamzungumzia binadamu na Maisha yake kwa ujumla. 

Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa na  Dr. Fred Luskin kutoka Stanford university yeye aliweza kugundua ya kwamba asilimia 65 ya watu wengi hawajui vipaji vyao na katika kundi kubwa la idadi hii ya watu ndio ambao wanafanya vitu ambavyo sio vyao, na asilimia 35 ambao ndio ambao wameweza kuvijua hivyo vipaji vyao haviwasadii katika maisha yao na wengine kwa asilimia 100, hii ni kutoka mafanikio yatokanayo vipaji hivyo huwa ni muda mrefu, na kwa kuwa watu wengi tunataka mafanikio ya muda mfupi uvumilivu hufika ukomo na kujikuta tunaviacha vitu hivyo na kuingia kufanya vitu vingine. Mfano mtu anakuwa na kipaji cha kucheza mpira katika timu kubwa hapa nchini na nje ya nchi,na kwa kuwa huenda umecheza kwa muda mrefu bila matarajio yake kutimia mtu huyo huacha kile ambacho hukifanya na kuamua kufanya kitu kingine ambacho sio kipaji chake mwishowe mtu huyo anajikuta anafanya hiki anakiacha mara kile nacho anakiacha. ukiona hicho unachokiita kipaji chako hakitoi burudani, hakifundishi, hakishangazi basi hicho sio kipaji. 

Namna ya gundua kipaji chako 

1. Kumuomba Mungu 
Hapa huwa pananifanya nimkumbuke sana samweli salali kwani aliwahi kuniambia ya kwamba kipaji ni kusudio la Mungu kwa kila mja wake. Kwani katika mafundisho yake katika vitabu vya dini vinasema kabla sijaumba nilikujua. Hii inamaana kila mwanadamu aliyeumbwa na Mungu ana kipaji chake, hivyo kinauwezo mkubwa wa kubadili maisha yake na jamii kwa ujumla, ila kipaji hicho watu wengi hawahujui mpaka dakika hii kuwa kipi kipaji chake ambacho Mungu kampa. Hivyo kama wewe ni miongoni mwa watu hao ni muda wako muafaka wa kutumia Muda huu kumuomba Mungu akuonyeshe kipaji chako. 

2. Marafiki, ndugu na wazazi 
Hili ni kundi muhimu sana ambalo litakusaidia wewe kujua kiapaji chako. Labda unaweza ukajiuliza ni kivipi? Tulia leo nipo kwa ajili yako. Watu ambao wanakuzunguka ndio wana Picha kamaili juu ya Picha kamaili ya maisha yako. Kwa mfano mtu akiwa mlevi hawezi kusema mimi ni mlevi ila watu ambao wanakuzunguka ndio ambao watasema yule jamaa ni mlevi sana. Picha hiyohiyo ya kumuona mtu mwingine tabia yake ndiyo ambayo inatumika kujua kipaji chako. Hebu waulize nyie mnanionaje, mna picha gani? Mnahisi nina kipaji Gani? Baada ya kuwauliza hayo wao ndio watakupa picha kamili juu ya kipaji chako na maisha yako kwa ujumla. 

3. changamoto 
changamoto ni njia nzuri ya bora sana ya kugundua kipaji chako. Ulimwegu wa leo ni ulikwengu wwnye changamoto nyingi sana, hata hivyo kutokana na suala hilo, pale matatizo yanapotokea na kuyapatia uvumbuzi sahihi hapo ndipo utakapojua kipaji chako. Kwa mfano watu wengi leo hii wanapenda Maisha ya kufanyiwa kila kitu. Mfano leo hii unamtegemea mtu fulani ili aweze kukutimizia lengo lako. Kwa mfano leo hii unafukuzwa nyumbani kwenu na kuambiwa nenda kajitegemee baada ya kuambiwa hivo ndipo unakujua kugundua ni kipi kipaji chako baadala  ya kwamba baadala ya kuendelea kuwa tegemezi. Hebu tuone mfano mwingine unakuta mtu alikuwa ni mfanyakazi wa ofisini ila baada ya kufukuzwa kazi unajikita unajikita  katika ufugaji mwisho wa siku unagundua wewe ulikuwa una kipaji kikubwa katika suala ufugaji badala ya kufanya kazi za maofisini. Hivyo wito wangu kwako ni vyema ukagundua kipaji chako mapema usisubiri changamoto fulani zitokee ndipo ugundue kipaji chako. 

4. Mashindano 
Kuna baadhi ya nchi huandaa mashindano mbalimbali kwa ajili ya kusaka vipaji, hili jambo jema sana hata hapa kwetu nchini kuna baadhi ya mashindano hufanyika amabayo husaidia kujua vipaji vya watu kama vile bongo star search, fiesta, DJ competion,  na mangineyo mengi. Hivyo kama kweli unataka kujua kipaji chako endapo yatatokea mashindano yoyote yale jitahidi sana kwenda kushiriki kwani hii itakusaidia kwa kiwango kikubwa kuweza kujua ni kipi kipaji chako. 

Mpaka kufikia hapo niweke nukta kwa kusema kama ukwisha kugundua hicho kipaji chako ni vyema ukajua ni namna gani ya kugeuza hicho kipaji chako kuwa pesa, kwani hapo ndipo palipo kuwa na changamoto kubwa. 

Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment