USIIPENDE SANA DUNIA NA VYOTE VILIVYOMO NA USIISAHAU SIKU YA HUKUMU.


Tazama vijana wanavyo upenda sana ulimwengu na Ibilisi anazidi kuwapokonya na kuwavuta kwenye maasi na uikataa haki na kuikimbilia batili”” Na pale utakapo washauri basi utawaona vijana wakiamaki na mda mwingine utaona wakitukana  lakini wanashidwa kujua kuwa maandiko hayawaruhusu kuipenda dunia. Ukisoma kwenye

Biblia 1YOHANA 2:15 -17   

15Msiupende ulimwengu wala mambo
yaliyoko ulimwenguni. Kama mtu yeyote
akiupenda ulimwengu, kumpenda Mwenyezi Mungu hakumo
ndani yake. 16Kwa maana kila kitu kilichomo
ulimwenguni, yaani, tamaa ya mwili, tamaa ya
macho na kiburi cha uzima, havitokani na Mwenyezi Mungu
bali hutokana na ulimwengu. 17Nao ulimwengu
unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye
afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele.

76. SURAT AL-INSAN
Kwa hakika watu hawa wanapenda maisha ya kidunia, na wanaiacha nyuma yao siku nzito
Qur’an 18: 45-49
Na wapigie mfano wa maisha ya dunia. Hayo ni kama maji tunayo yateremsha kutoka mbinguni, yakachanganyika na mimea ya ardhi, kisha hiyo mimea ikawa vibuwa vinavyo peperushwa na upepo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.
 
46. Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia. Na mema yanayo bakia ni bora mbele ya Mola wako Mlezi kwa malipo, na bora kwa matumaini.
 
47. Na siku tutapo iondoa milima na ukaiona ardhi iwazi, na tukawafufua - wala hatutamwacha hata mmoja kati yao
 
48. Na wakahudhurishwa mbele ya Mola wako Mlezi kwa safu (wakaambiwa): Mmetujia kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza! Bali mlidai kwamba hatutakuwekeeni miadi.
 
49. Na kitawekwa kitabu. Basi utawaona wakosefu wanavyo ogopa kwa yale yaliomo humo. Na watasema: Ole wetu! Kitabu hichi kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa ila huliandika? Na watayakuta yote waliyo yatenda yamehudhuria hapo. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote.


LUKA 18:29-30

29Yesu akajibu, “Amini nawaambia, hakuna
hata mmoja aliyeacha nyumba yake, au mke,
au ndugu, au wazazi au watoto kwa ajili ya
Ufalme wa Mungu 30 ambaye hatapewa mara
nyingi zaidi ya hivyo katika maisha haya na
hatimaye kupata uzima wa milele ujao.’’

8. SURAT AL-ANFAAL


72. Hakika wale walio amini na wakahama na wakapigania Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao, na wale walio toa mahala pa kukaa, na wakanusuru, hao ni marafiki na walinzi wao kwa wao. Na wale walio amini lakini hawakuhama, nyinyi hamna waajibu wa ulinzi kwao hata kidogo mpaka wahame. Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia, isipo kuwa juu ya watu ambao yapo mapatano baina yenu na wao. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.




Share on Google Plus

About DAIMA ANGAZA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

1 comments: